Home Ligi LA LIGA Madrid Watampiga Chura Teke Au Watamwacha Mwanaharamu Apite?

Madrid Watampiga Chura Teke Au Watamwacha Mwanaharamu Apite?

6952
0
SHARE

Real Madrid wanawapokea Atletico Madrid pale Bernabeu. Ni maamuzi yao aidha kutoa nafasi kubwa ya kombe kwa Barcelona na kuwaekeka kwa gwaride la heshima kwenye mchezo ujao au kumwachia Atletico azidi kumfukuzia Barcelona.

Ishu nzima ipo hivi.

Barcelona Atletico Madrid Real Madrid
Michezo 31 Michezo 30 Michezo 30
79 67 63

Kama Real atashinda atafikisha alama 66 na atakuwa amebakiza alama 13 kuifikia Barcelona. Maana yake atatoa mwanga kwa Barcelona kuzidi kuchanja mbuga kwani atahitaji kushinda michezo minne kutawazwa bingwa. Michezo minne ya Barcelona ijayao ni dhidi ya Valencia, Celta Vigo Sevilla na kwenye mchezo wa Deportivo ndio utakaompa Barcelona ubingwa. Mchezo unaofuta ni dhidi ya Madrid na itabidi waweke gwaride. Alama zilizobakia mpaka mwisho wa wa msimu ni 21 tu. Barcelona watahitaji Atletico apoteze mchezo wa leo na kisha watakuwa na jukumu la kutafuta alama 10 kwenye michezo minne kabla ya kukutana na Madrid na kupewa heshima hiyo.

Madrid hali zao zipoje?

Wapo nyuma ya alama 16 nyuma ya Barcelona. Itakuwa fedheha kubwa kama Ronaldo atashindwa kutikisa nyavu leo. Mshindani wake mkubwa Messi jana amefunga magoli matatu bila shaka yupo nyuma ya magoli 7. Ronaaldo ameifunga Atletico magoli 21 katika michezo 30 na kuweka historia ya mchezaji aliyewahi kufunga magoli mengi katika dabi hiyo.

Taarifa za timu

Real Madrid

Kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha ya Nacho anapata jeraha, amepatwa na matatizo ya misuli. Ikumbukwe vyema katika maisha ya soka la wakubwa nacho hhawahi kuumia. Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa Varane kuanza katika mchezo huu. Hakuna mchezaji hata mmoja mwenye adhabu wote wapo fiti kuanza.

Atletico Madrid

Junafran amerejea tena kikosini, Felipe Luisihatocheza kabisa mchezo huu, Sime Vrsaljko na Jose Gimenez wapo kwenye uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo huu.

PATA KIFURUSHI

 

Hii itakuwa dabi ya 219, Wote wameshinda mara 109

Real Madrid imeshindwa, Kushinda michezo yake

Minne ya Mwisho dhidi ya Atletico

Katika uwanja wao wa Bernabeu

Wamdroo mmoja na Kufungwa mitatu 

 

Madrid imepiga mashuti mengi yaliyoelekea golini kuliko klabu nyingine yeyote (228)

Hata hivyo klabu iliyoruhusu kupigiwa mashuti machache golini ni Barcelona mashuti (94) na Atletico imepigiwa mashuti yaliyolenga lango mashuti (96).

Kauli za Makocha

Simeoni Amewataka vijana hawa wa Los Merengues kujituma kuhakikisha wanatia presha kubwa zaidi majirani zao wa katalunya. “tunakikosi ambacho kila siku ni kilekile, hatubadiliki sana, tutajaribu kushinda kwa kuangalia umoja wetu na sio mchezaji mmoja mmoja, sina uhakika sana kama Madrid wana timu bora duniani ila nachojua wana kikosi bora kizuri”

kauli hii ina ukakasi. Anachomaanisha kuwa Madrid wanakikosi kizuri kwa kuangalia mchezo mmoja mmoja ila haoni kama wana timu nzuri hasa tukiangalia muunganiko wake. Nadhani matazamo wake huu amelenga zaidi mashindano ya ligi kuu ambayo ni kigezo msingi zaidi cha kupiga ubora wa timu na sio ubora wa mchezaji mmoja mmoja. Alipoulizwa kuhusu goli la Ronaldo alisema “nawaza kama mshabiki mwingine yeyote, lile goli ni la maajabu”

Zidane alipoulizwa vipi kuhusu mchezo huu ni nani mwenye faida kubwa nao, amejibu ni mchezo muhimu kwa pande zote. Ni wazi anachokitafuta ni ushindi tu.

Kachumbari

Mwandishi: je utaweka gwaride la heshima pale Camp Nou endapo Barcelona watatwaa ubingwa?

Zidane; kwanini mnaniuliza hili swali kila siku? Nishasema, hatutafanya hicho kitu, ni maamuzi yangu, wala sitambui hicho mnachosema gwaride la heshima, nishaamua, sitofanya hicho kitu. Wao (Barcelona) waliharibu huu utamaduni.

Zidane ana gubu au Barcelona wana nongwa? Gwaride la heshima sio tu utamaduni ila ni heshima ambayo hata Barcelona waliwahi kufanya kkwa Madrid. Gwaride la heshima halipo tu kwa mashindano ya ndani. Mwaka 2008 Barcelona iliweka gwaride la heshima kwa Real Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa la liga. Pia Barcelona waliwafanyia Sevilla gwaride la heshima baada ya kutwa kombe la UEFA mwaka 2006. Je kwanini waligoma kuwafanyia hivyo Real Madrid baada ya kutwaa kombe dunia la vilabu?

Lakini Guilermo Amor aliwajibu kuwa hawawezi kumpa mtu heshima mashindano ambayo wao hawajashiriki. kimsingi Amor alikurupuka kwani mwaka 2006 waliwafanyia hivyo Seville wakati hawakushiriki kombe hilo.

 

Kwa taarifa yako

Mara ya mwisho Madrid kushinda Bernabeu ilikuwa mwaka 2012, wakati huo kepteni alikuwa Iker Casilas. Kwenye kombe la klabu bingwa wamekutana mara 4 na Atletico amepigwa mechi zote 4. Antonio Griezmann ameshafunga magoli matano dhidi ya Madrid (mawili akiwa na Atletico). Kama atafungwa mchezo huu wa leo atakuwa mchezaji wa kwanza katika karne hii kufunga goli katika michezo mitatu dhidi ya Madrid mfululizo.

Wapinzani hawa wa jadi?

Mashabiki wa Atletico wamekuwa wakiwatania mashabiki wa Madrid kuwa hawajielewi, lakini hata hivyo mashabiki wa Madrid wamekuwa wakawazodoa mashabiki wa Atletico kuwa hawajiwezi.

Kioja

Laurence and François Hernández mt0to wao mmoja Lucas atakuwa anaichezea Atletico, mtoto wao mwingine yupo Real Madrid (Theo). Furaha kubwa kabisa katika familia hii. Ingawa watoto wote wanasema huwa hawaongeleagi masuala ya dabi nyumbani lakini haiwazuii leo kupambania vilabu vyao.

imeandaliwa na Privaldinho (instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here