Home Kitaifa kwani Yanga na Welayta kuliendaje?

kwani Yanga na Welayta kuliendaje?

8323
0
SHARE

Mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Yanga na Wolayta Dicha SC kutoka Ethiopia umekamilika. Yanga waliweza kupata ushindi wa magoli mawili kwa bila na kujiweka mguu mmoja mbela katika hatua ya makundi. wahabeshi walishindwa kabisa kuipenya ngome ya Dante na Ninja. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yalijitokeza katika mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Yanga na Welayta Dicha.

Walinda lango?

Youthe Rostand aliweza kuchomoa michomo minne licha ya kufanya uzembe mara moja. Golikipa wa Wolayta Wondwosen Geremew aliokoa mipira mitatu na hakufanya uzembe wa aina yoyote.

Safu za ulinzi zilikuwaje?

Timu zote zilikuwa imara katika kuzuia mashuti. Yanga waliweza kuzuia (kublock) mashuti 6, Welayita walizuia mara 6. Andrew Vicent Dante na Abdal shaibu Ninja walifanya kazi ya ziada kwa kuhakikisha mkameruni hatari Arafat Djako na Yared Dawit Yarfo kuonekana kama watazamaji tu. Yanga waliweza kuondosha mashambulizi yaliyonekana kuwa namadhara makubwa katika eneo la hatari mara 10 huku waethiopia wakiondosha mara 4.

PATA KIFURUSHI

Jina la Utani Bees of Tona

Uwanja wao Wolayta Sodo

Kocha; Zenebe Fisseha

Umiliki wa mpira na Eneo la kiungo

Bila shaka Wwaethiopia walitawala sana eneo la kiungo kwani walikuwa na uwezo mzuri wa kumiliki mpira. mchezo wao mwisho dhidi ya Zamalek kocha wao aliwaambia waandishi ha habari kuwa hawataenda kuzuia ugenini mara baaa ya kupata ushindi nyumbani. Kocha huyu mpya wa Wolayta dicha anaoenakana kuwa anajiamini sana.

Katika mchezo huu Yanga walitumia zaidi mipira mirefu ili kuwatafuta washambuliaji wao. Yanga walicheza mipira mirefu ya malengo mara 24 huku Welayta Dicha wao kipindi cha kwanza hawakucheza mipira mirefu sana lakini kipindi cha pili baada ya kuona hali mbaya walibadilisha mfumo wao na kuacha mipira mirefu mara 9.

Mara ya mwisho Yanga kufuzu hatua ya makundi ilikuwa mwaka 2016 ilipopangwa na Medeama (Ghana), TP Mazembe (DRC Congo), na Mo Bejaia (Algeria).

Safu ya ushambuliaji.

Ibrahim Ajibu pamoja na Yusuph Mhilu walijitahidi sana kutengeneza nafasi nyingi za magoli. Yanga walitengeneza nafasi muhimu takribani 13 huku wapinzani wao wakitengeneza nafasi 4. Yanga walipiga mashuti takribani mashuti 14 na mashuti 4 yalilenga golini, Welayta wakapiga mashuti 8 na 5 yalielekezwa kwenye lango la Yanga. Yanga walifanikiwa kupata kona 7 sawa na welayta. Yanga walifika langoni mwa Welayta nara 73 huku Welayta wao wakijaribu mara 65.

Nidhamu ya mchezo.

Mpira ulikuwa mzuri na kuvutia. Hakukuwa na zile rabsha za vurugu kutokana na mfumowa wapinzani wa Yanga. a. Aina hii ya mchezo ulifanya mchezo kutulia kwani Yanga waligundua tatizo la Welayta. Yanga walicheza rafu mara 9 na Welayta nao walipata. Hakukuwa na kadi na ni mchezaji mmoja tu aliyetolewa nje kwa majeraha.

Ilikuwaje Yanga wakafanikiwa? Wapinzani wa Yanga walikuwa na miili midogo sana. Walicheza mchezo wa pasi nyingi ili kukwepa mpira wa nguvu kwani hawakuwa na miili ya kucheza aina hiyo ya mpira. Kimo cha wachezaji hawa wa Welayta ndio alikuwa mchawi wao. Yanga walifanikiwa kupiga krosi 15 na krosi mbili zilazaa matunda. Welayta sio warefu ni wafupi na Yanga waligunuda hilo mapema. Yanga wanapaswa kutumia mfumo huo wa mipira ya juu kule sodo stadium

Uzuri wa Welayta?

Walianza kwa mbwembwe sana, wakawa makini kwenye upigaji wao wa pasi. Walikuwa na wastani wa pasi 10 kwenye nusu ya uwanja wa Yanga, huku yanga wakiwa na wastani wa pasi tano pekee kwenye nusu ya upande wa Welayta hasa kwa kipindi cha kwanza. Walikuwa wanabembeleza sana. Na walichelewa kubadilika kwani walicheza kwa kujiamini kiasi cha kupitiliza.

Ushauri?

Yanga wawe makini sana katika mchezo wa marudiano. Takwimu zao zinaonesha kuwa michezo yao minne ya mwisho hawajapoteza nyumbani.

Takwimu zote na makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram) (0763370020)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here