Home Kimataifa Mambo 5 ambayo yananipeleka Escape One hii leo, washtue wana muje tuonane...

Mambo 5 ambayo yananipeleka Escape One hii leo, washtue wana muje tuonane baadae

7814
0
SHARE

Huku Manchester City vs Manchester United, pale Everton vs Liverpool, leo mapemaaa na jezi ya chama langu Coastal Union ya Tanga nitakuwa Escape One kuangalia watu wakitoana jasho, lakini hata kama sina timu ila mambo haya 5 yananifanya niende Escape One.

1.Mourinho atakubali United wadhalilike. Hivi umeshawahi kuona kocha kiburi kama Mourinho? Hakubali kufungwa na hapendi kudhalilika. Kama City wakimfunga Mou baasi watatangaza ubingwa lakini mimi nataka kuona kama Jose atakubali kirahisi hili litokee.

2.Klopp kuendeleza uonevu kwa Everton au Allardayce atakataa. Katika michezo 16 katika michezo tofauti ambayo Liverpool amecheza na Everton, Liverpool wameshinda michezo 8 na kusuluhu 8(hawajapoteza), lakini kibarua cha Sam Allardayce kiko mashakani na akiisimamisha Liverpool kwa kiasi fulani atakaa pazuri.

3.Liverpool bila Mo Salah. Hakuna mwenye uhakika kama Mo Salah atakuwepo leo katika mechi dhidi ya Everton kutokana na mejeruhi aliyonayo, amekuwa kinara wa mabao na leo akiwepo akafunga atakuwa na mabao 30 na kuwa Muafrika wa kwanza kufikisha mabao hayo Epl kwa msimu mmoja, lakini je asipokuwepo watachezaje? Nataka kuona namna Klopp anavyoweza kutuaminisha wao hata bila ya Salah wako fiti.

4.Alexis Sanchez anioneshe kama sio mwizi.Ni mchezaji anayelipwa zaidi United, lakini tangu ajiunge na United hajawa na kiwango ambacho United wanakitaka, wanasema mchezo mkubwa ni kwa wachezaji wakubwa na huu ndio mchezo Sanchez atuoneshe kama kweli amestahili kuwa mchezaji anayelipwa zaidi United.

5.Ni basi au Mou atajitutumua Etihad? Mourinho anatajwa kama adui wa soka, hii ni kutokana na mchezo wake wa kujilinda katika michezo kama hii, lakini kuashambulia City ni approach sahihi zaidi hii leo, natamani kuona kama Mou atashambulia kama Klopp alichofanga juzi au ataogopa na kupaki basi ambalo ni wazo hatari mno hii leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here