Home Uncategorized Kadi nyekundu zinanipeleka Escape One kuiona Everton vs Liverpool leo

Kadi nyekundu zinanipeleka Escape One kuiona Everton vs Liverpool leo

6714
0
SHARE

Kama ulikuwa hujui tu ni hivi, hakuna mechi yoyote ya EPL inaongoza kwa kadi nyekundu kama mchezo Marseyside Derby, huu ndio mchezo ambao hadi sasa kumewahi kutolewa kadi nyekundu 21.

Katika kadi hizo sasa 21,kumetolewa kadi 14 kwa Everton pekee na hii inawafanya timu ambayo inaongoza kwa kupokea kadi nyingi nyekundu dhidi ya mpinzani mmoja katika historia ya ligi ya EPL.

Hili ndio soka tunapenda vijana wa sasa soka la utemi, na leo tena tunakwenda kuona vita kubwa katika mchezo huu na sio ajabu kadi nyekundu zikaendelea kutembea, siwezi kukosa kwakweli mechi ya kitemi namna hii, ndio maana leo mapemaaa nitakuwa Escape One pale Mikocheni.

Liverpool wamepoteza mechi 2 tu katika mechi 11 za mwisho za ugenini katika EPL humu Mo Salah kama hii leo akifunga bao atakuwa Muafrika wa  kwanza kufunga mabao 30 katika msimu mmoja wa EPL.

Katika siku za usoni Everton wamekuwa wachovu sana kwa Liverpool, katika michezo 22 iliyopita baina ya timu hizi mbili, Everton wameshinda mechi 1 tu wakapigwa 11 na kwenda suluhu mechi 10.

Katika michezo 16 ya mwisho ambayo Liverpool na Everton wamekutana katika michezo yote, Liverpool hajapoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa wameshinda michezo 8 na michezo 8 iliyobaki wakitoka suluhu.

Katika vipigo 8 vya mwisho ambavyo Everton wamepigwa katika dimba la Goodison Park, vipigo 7 vimetoka katika timu ambazo zinatokea kwenye top 6 ya EPL huku kipigo kimoja kilichobaki wakipewa na Burnley.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here