Home Kimataifa Kabla hatujaenda Escape One, tujikumbushe timu ambazo zilibeba EPL mbele ya wapinzani...

Kabla hatujaenda Escape One, tujikumbushe timu ambazo zilibeba EPL mbele ya wapinzani wao wakubwa

10872
0
SHARE

Kama leo City watawapiga United baasi shughuli ya ubingwa itakuwa imeishia hapo na City watakuwa mabingwa wapya EPL, City wanatwaa kombe hili huku wakiwa na michezo 6 mkononi ambayo haijapigwa bado.

Manchester United ndio klabu inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huku zikiwa bado mechi nyingi, ilikuwa msimu wa 2000/2001 ambapo United walibeba ndoo huku ikiwa imebaki michezo 5 ya ligi.

Lakini kuelekea mchezo huu wa leo achilia mbali City wanaweza beba kombe zikiwa zimebaki mechi nyingi lakini pia Man City watabeba kombe kwa kuwafunga wapinzani wao wakuu, tuone timu ambazo zimewahi kufanya kile City wanachotaka kufanya.

1988/1989 Arsenal kwa Liverpool, achana na hii ambayo City wanabeba wakiwa nyumbani, Arsenal msimu wa 1988/1989 walibeba ubingwa wa EPL mbele ya Liverpool(tena Liva wakiwa nyumbani) katika hali ambayo wengi hawakutaraji.

Mechi hii Arsenal walihitaji kuifunga Liverpool bao zaidi ya 1 ili kuwa mabingwa, na uwezo wa Liverpool ulionesha ni ngumu kufungwa mabao hayo. Dakika ya 52 ya mchezo Alan Smith aliwapa Gunners bao la kuongoza na dakika za lala salama Michael Thomas akafunga lingine na Gunners wakawa mabingwa Anfield.

2001/2002 Arsenal wanabeba ndoo Old Traford. Hakuna kitu mashabiki wa Gunners wa ukanda wa Afrika wangeshangilia kama tukio hili, kuifunga United Old Traford na kisha kutangaza ubingwa mbele yao.

Hakuwepo Thiery Henry, wala hakuwepo Tony Adams lakini Gunners waliipiga United bao 1 kwa nunge pale OT na siku hiyo wakatangazwa kuwa mabingwa wapya wa EPL kwa msimu wa mwaka 2001/2002.

2003/2004 Arsenal anashinda White Art Lane. Sasa wana Arsenal kindakindaki nchini Uingereza hii ndio hadithi ambayo wanamhadithia kila mtu kuhusu walivyowahi kuwa mabingwa, hadithi yao tamu zaidi.

Ni hadithi tamu sana kwa Arsenal kutangazwa kuwa mabingwa katika dimba wanalolichukia zaidi ambalo ni White Art Lane. Hawakushinda hii mechi lakini suluhu ya 2-2 dhidi ya Tottenham iliwahakikishia ubingwa wa EPL 2003/2004.

2005/2006 Chelsea anashinda mbele ya United. Kabla ya Mourinho kwenda United alikuwa kati ya maadui wakubwa sana wa mashabiki wa United. Mambo yake na maneno yake vilileta uadui na chuki kati yao.

Tukio la 2005/2006 la Mou kuwarushia mashabiki medali yake baada ya ubingwa walioupata kwa kuipiga United mabao 3 kwa 0 linatafsiriwa kama tukio la kebehi sana kwa mashabiki wa United.

Hizo ni mechi ambazo bingwa aliupata kwa kumchapa mpinzani wake, leo vipi Manchester City atampiga United na kuwa mabingwa wapya EPL au Mourinho atakataa? TUONANE ESCAPE ONE BAADAE.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here