Home Kimataifa Road To World Cup “Top 5 ya wachezaji wanaoongoza kwa kadi kombe...

Road To World Cup “Top 5 ya wachezaji wanaoongoza kwa kadi kombe la dunia”

7843
0
SHARE

Bado siku chache tu kwa michuano ya kombe la dunia kuanza, rekodi mbali mbali bado zipo kuelekea michuano hii, lakini leo tuone nyota 5 wenye kadi nyingi zaidi katika michuano ya kombela dunia.

5. Tim Cahill, moja kati ya wachezaji maarufu zaidi kuwahi kutokea nchini Australia ni Tim Cahill, lakini huyu ni kati ya wachezaji wanaotumia nguvu sana uwanjani na haishangazi hadi sasa kuwa na kadi 4 za njano.

4.Rigobert Song. Mchezaji pekee wa Africa aliyeko katika orodha hii,nyota huyu wa zamani wa Cameroon kama ilivyo kwa Cahill naye pia ni mchezaji ambaye ana kadi 4 za njano alizozipata katika mechi 9 alizocheza.

3.Cafu. Kati ya walinzi bora kabisa kuwahi kutokea Brazil, na katika World Cup 4 alizowahi kucheza amefanikiwa kubeba mara mbili, lakini mlinzi huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil amepewa kadi 6 za njano katika mechi 20 za World Cup alizocheza.

2.Rafael Marquez. Hii ilikuwa ni roho ya Mexico, Marquez alikuwa akipendwa sana na mashabiki wa timu ya soka ya Mexico kutokana na kujitoa kwake timu ya taifa, katika michezo 16 ambayo Marquez ameichezea Mexico amepewa kadi za njano 5 na nyekundu 1.

1.Zinedine Zidane. Katika viungo bora waliowahi kuonekana duniani, ukitaja watatu jina la Zidane lipo, uwezo wake uwanjani kila mtu ameuona. Lakini pamoja na hayo ula Zidane anaongoza kwa kupewa kadi, michezo yake 12 kwa Ufaransa Zidane amepewa njano 4 na nyekundu 2, huku kadi yake maarufu zaidi ilikuwa mwaka 2006 baada ya kumpiga kichwa Marco Materazzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here