Home Ligi EPL Mourinho Vs Guardiola: niliyaona haya kitambo

Mourinho Vs Guardiola: niliyaona haya kitambo

15309
0
SHARE

Makala hii niliandika tarehe 31 mwezi wa kwanza mwaka 2016.

Nilichokiona kwenye akili yangu kuwa kama Mourinho na Guardiola watakuwa ligi Moja basi tutarajie wao tu kutawala. Lakini pia nilitabiri kiama cha Chelsea. Hata hivyo nilijua tu baadhi ya tabia za Mourinho zitaiathiri sana Man United.

Nilianza hivi…

Ugonjwa wa Mourinho ni kwamba, ana mafanikio ya muda mfupi, lakini mambo yanapokwama huwa anaanza kuwasakama watu wanaomzunguka na ataanza kunyoosha vidole ovyo na ufalme wake utaanza kuporomoka ghafla, kingine ataanza kunyanyasa wachezaji wadogo na wasiocheza mpira wa nguvu (Tumekwisha ona migogoro yake na Martial na shaw na hata micky Pogba na Mata)…

TURUDI NYUMA KIDOGO
Watu wengi wanajiuliza kwanini Inasemekana palikuwepo na Ugomvi kati ya Pep Guaardiola na Marehemu Tito Villanova? Huwa watu wanasema tusimseme Vibaya Marehemu . Wakati ule Tito alikuwa akifanya kazi na Pep Guardiola pale Barcelona walikubaliana kuwa watasitisha vibarua vyao na kutimkia United. Lakini mara baada ya Guardiola kutangaza kung’ooka Barcelona alishangazwa na taarifa kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wake Bw. Titto Villanova ametajwa kuwa kocha mkuu wa Barca.

Tuendelee….

Guardiola alikereka sana na kitendo kile, kisha alielekea zake Marekani kula Bata na kupumzika. Wadadisi wa mambo wanadai alimkimbia Mourinho na wengine wanadai walishindwa kuelewana na mabosi. Baadae Tito aliiugua sana, mbali na ugomvi wao Guardiola alienda Kumuona Tito hospitalini mara moja.

Wakati ule Sir Alex Ferguson alifanya mikutano zaidi ya 12 na Pep kule marekani akimsihi ajiunge na Man utd. Baadae Ferguson alizubaa mwisho wa siku Pep alijunga Bayern Munichen. Tageti ya mwisho ya Fergie kupata mrithi wake alikuwa Bw Jose Mourinho. Dili hili nalo lilikwama

Mkasa wake na Abramovich

2007 mourinho alimalizana na Chelsea lakini makubaliano yao ni kwamba asirudi timu yoyote England kwa wakati ule. Kwa mara nyingine Mwaka 2015 Mourinho alimalizana na Chelsea lakini mkataba wake raundi hii haumbani kufundisha klabu yoyote pale Uingereza. Abramovich amesahau kuwa Man utd na Man city zina njaa ya makocha. Amesahau pia Pep Guardiola amevunja mkataba na yupo njiani kuja Uingereza na mwisho anajifanya kuwa hajui kama Brenden Rodgers amempisha Klopp.

NANI KAMLOGA ABRAMOVICH?

Kwanini nasema Abramovich amejisahau, nawaza tu, hivi Mourinho akienda United, halafu Guardiola aende Man city? Maana yake nini? Hata kama Chelsea atapata kocha mwingine akatwaa ubingwa lakini bado siku zijazo watatesekana. Mourinho na Guardiola watahitaji mwaka mmoja tu kujegna timu zao. Baada ya hapo nani atasimama mbele yao?

Kimsingi Chelsea itakuwa underdog (yaani tunasema Chelsea itakuwa timu ndogo mbele ya mafahali hawa)

kwanini nasema Chelsea watakuwa Underdog?

Ni hivi…
Tokea 2002 Mourinho amefundisha timu 5 tofauti na kote alibeba ubingwa wa ligi, na kote alitawala na kubadili upepo wa ligi. Sitaki kumzungumzia sana Guardiola maana hilo lipo wazi, je kama hawa watu wakiwa England nani atakuwa underdog (kilaza) si chelsea? Au nawaonea? Ni kocha yupi atapambana na hawa wanaume? Ni kocha yupi atakaeikoa Chelsea midomoni mwa Klopp, Wenger, Pep na Mourinho? Ndugu zangu nawasihi kwenye sala za jioni na za asubuhi mkumbuke kuiombea chelsea.

MOURINHO VS GUARDIOLA Tuachane na hayo, nachoamini vita itabaki kwa Pep na Mourinho, kwa upande fulani endapo Pep ataenda Man city Pep binafsi yangu yeye ndo atakuwa underdog hasa kwenye msimu wa kwanza, kwanini nasema atakuwa underdog, mfumo wa Pep Guardiola hauwezi kufanya kazi EPL kwa haraka. Itamchukua muda kidogo.

EPL unahitaji kasi, nguvu na akili, sio uwezo binafsi wa Pasi wala chenga. Itambidi atafute mabeki wenye nguvu na kasi ili kuweza kumsaidia viungo wake kucheza kwa kujiamini hapo ndipo mfumo wake utafanya kazi. Rafiki yangu mmoja aliniuliza je mfumo wake ukikubali? Nilimjibu kwamba sio Mourinho tu atapoteaana ila ligi nzima itafyata mkia. Pep ni mastermind (akili nyingi) Nawaza sana Pep akifanikiwa kucheza mpira wa Pasi nyingi Pale Britania stadium na akapata matokeo ni nani atainuka kumzuia? Kazi ipo. Narudia tena kama mfumo huu utakubali basi ataitawala EPL vibaya mno.

Mourinho Man United
Watu wanasema Mourinho huwa mafanikio yake ni ya gharama na ya muda mfupi! Swali ni je kwa gharama walizotumia united wataendelea kumwaga tena pesa? Labda.. Lakini nachoona itamchukua muda kubadili mfumo wa Man utd kwa sasa! United wanacheza mfumo wa akina Guardiola kwa sasa, Mou akija lazima abadilishe, na huko ni kuwavuruga wachezaji. Mourinho hawezi kucheza mfumo wa pasi kamwe.

Bado atataka kuleta wachezaji wake? Lakini usisahau kuwa usajili ni kamari angalia hawa watu, Mo salah, Juan Quadrado, Andrei Shurrle, Kelvin De bruyne, hapa kote Mourinho alipoteana. Kwa mantiki hiyo atataka kubadili mfumo na kujenga himaya yake, pili atataka kuleta watu wake pia mfumo unaweza ukawakataa.

Hivyo Man utd wataingia kwenye kamari ambayo kocha wa zamani Bw. Atkinson, na mchezaji wa zaman Bobby Chalton wanaikataa. Hawamtaki kabisa Mourinho na wanamtaka zaidi Pep ambaye hatobadili mfumo ila ataongeza ujuzi wake tu . Najua Fergie anachanganyikiwa maana anafahamu Mou ni mpita njia, na anajua wazi kuwa Bodi ya Man utd haimtaki.

Karata inayomweka Louis Van gaal mjini. Sijui mwisho wa hii filamu ila kilio changu ni saala kwa ndugu zangu wa darajani

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here