Home Ligi EPL Wachezaji wa Man City wanahuzunisha

Wachezaji wa Man City wanahuzunisha

17371
0
SHARE

Mapema hivi leo wachezaji wa Manchester City wamerudi mazoezin kwa ajili ya kujiandaa na Mchezo wao dhidi ya Man United. Picha zifuatazo zinaonesha wachezaji wa City wakielekea kwenye uwanjan wa mazoezi

Baadhi ya nyuso zao hazikuwa na ushirikiano kabisa. Wameonekana kuchoshwa kabisa na matokeo ya Liverpool

Otamend alishindwa kabisa kusimama imara na mwenzake Laporte kuhakikisha ngome yao haipenyeki. Mawazo yao kwa sasa yapo mbali kabisa. Hawana hamu. Ni kipigo ambacho hawakutarajia kabisa.

Raheem Sterling aliingia kipindi cha pili kwa kuchukua Nafasi ya Ilkay Gundogan. Mashabiki wa Liverpool walikuwa wakimzomea sana. Jitihada zake hazikuzaa matunda.

Gabriel Jesus nae amefika mazoezini. Alicheza chini ya kiwango baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Van Djik. Matarajio yao hayakwenda sana. Kuna uwezekano mkubwa hana maelewano mazuri na Leroy Sane kiuchezaji na kimfumo. Mara kadhaa tumewaona wakirushiana mikono.

Guardiola amesema haoni wa kumlaumu. Ni matokeo ya kawaida. Walijitahidi kutengeneza nafasi lakini bahati haikuwa yao.

De bruyne amesema wanahitaji nguvu ya ziada. Anaamini hawakucheza vibaya lakini unapofungwa magoli matatu hakuna anayejali ulicheza vipi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here