Home Kitaifa Ukurasa wa Ally Hamad Ally kijana wa Manji mwenye kipaji

Ukurasa wa Ally Hamad Ally kijana wa Manji mwenye kipaji

14002
0
SHARE

“Tatizo kubwa linalokwamisha ligi yetu ni Kwa vilabu Vidogo namna vilabu hivi vinavyofanya kazi. Wachezaji wengi wanakata tamaa kutokana na matatizo ya mishahara. Wakati fulani mchezaji unacheza kama miezi mitatu unajituma lakini hupewi mshahara au mshahara unakuja nusu. Ni tofauti na vilabu vikubwa maana wao hata wasipopewa mishahara kwa wakati lakini posho bado kwao zipo”

Hayo hayakuwa maneno yangu ni Maneno ya Beki kisiki wa stand United Ally Ally.

Beki huyu aliyezolea jina kubwa katika kikosi cha Stand United ni moja ya wachezaji wanaonesha kiwango kizuri sana kutokea visiwani (Zanzibar).

Wasifu wake


Majina Ally Hamad Ally
Alizaliwa mwaka 1994
Mahali: Gulioni Kariakoo Zanzibar
Katika Hospitali ya Mwembeladu

Anajulikana kwa jina la Utani kama mwarabu. Amezaliwa katika familia ya kipato cha kawaida. Baba yake alicheza soka lakini sio soka la ushindani kwa sababu hakuwahi kuwa na malengo na soka. Ally mwenyewe hakuwahi kuwa na Malengo kabisa na Soka. Alicheza soka shuleni kabla hajaamua kuachana na shule mwaka 2011 akiwa kidato cha Pili. Shule ya Sekondari Mwembeshauri iliyopo maeneo ya kariakoo.

Kuanzia 2011
Baada ya kuachana na shule aliamua kujikita kwenye soka licha ya kwamba alikuwa mvivu sana mazoezini. Alianzia mazoezi ya kisoka katika kituo kimoja kilichopo Mkunazini. Kituoni alikorifishana sana na waalimu wake kutokana na uvivu wake na utovu wa nidhamu. Alikuwa na kiwango kizuri kwenye timu kitendo kilichomfanya awe anaringa hata kwenda kwenye mazoezi. Licha ya uvivu wake kiwango kiliimarika maradufu ndipo klabu ya ligi daraja la pili lilipomchukua.

Ajiunga na Vikokotoni mwaka 2012
Baada ya kukaa kwenye kambi ya Mkunazini mabosi wa vikokotoni walihitaji huduma zake. Aliichezea klabu hiyo kwa mwaka mmoja na nusu. Kwenye akili yake hakuwa na malengo yoyote na mpira. Hulka ile ilidumaza sana ufanisi wake. Alicheza tu kwa sababu watu walimtaka afanye hivyo.

Atupwa Gulioni 2014
Baada ya misukosuko kadhaa aliamua kwenda klabu yake ya nyumbani ya Gulioni ambayo ilikuwa ligi daraja la tatu. Aliamua kujiunga na Gulioni kwa sababu ilikuwa kwenye hatari ya kushuka Daraja la 4. Aliipigania klabu yake hatimaye ikapanda daraja la Pili.

“Kwenye maisha watu wakiona unataka kufanikiwa wanajitokeza kukushauri sana. Huwa najiuliza walikuwa wapi hapo awali. Kila mtu alikuja na ushauri wake. Mtu pekee niliyekuwa namsikiliza ni Kamal Manji” anasema Manji kwake ni kama Baba.

Baada ya hapo aliamua kuweka malengo. Moja ya lengo lake kuu alisema “nilijiambia kuwa lazima watu wanitazame kwenye TV nacheza mpira. Sitaki kucheza ligi kuu ya Zanzibar nataka kwenda Bara huko ndiko nitaonekana”

Safari yake ya Stand 2016
Mwaka 2016 Stand United ilikuwa na tatizo kubwa la kiuchumi. Tatizo hili lilirudisha nyuma uwezo wa klabu kuweza kununua wachezaji. Klabu hiyo ilianzisha mfumo wa Majaribio kwa wachezaji wasiokuwa na mikataba popote. Kila mchezaji alialikwa kwenda kuonesha uwezo. Huu ulikuwa wakati muafaka wa Ally Ally kuonesha cheche zake.

Mchezo wake wa kwanza tu wa majaribio ulimpeleka kwenye kikosi cha Stand United.
“Nakumbuka nilifanya mchezo wa majaribio na Timu yetu ilikuwa ikicheza na timu ndogo ambayo tuliitangulia mbele magoli mawili.

Nilipata jeraha na mwalimu aliamua kunitoa nje. Nilipotoka nje timu yetu ilirudishiwa magoli yote. Niliumia sana. Mwalimu alinifuata na kuniambia kuanza sasa wewe ni mchezaji wa Stand United. Nilifurahi sana. Niliporudi kambini nilipewa Chumba changu. Nikampigia Simu Manji nikamweleza kuwa nimefaulu. Bosi Manji alifurahi sana.

Maisha yake Stand
Maisha ya Stand yalikuwa magumu sana kutokana na upweke. Rafiki yangu alikuwa ni Ambrosse ambaye kwa sasa hachezi Stand. Ally anaeleza kuwa shida kubwa ilikuwa ni wachezaji kukosa uvumilivu. Wachezaji wengi waliondoka kutokana na ugumu wa maisha. Mbaya zaidi mimi mwenyewe sikuwa na mkataba na timu hii.

Kwanini hukuwa na mkataba?
Baadhi ya viongozi Stand walikuwa hawapendi ninavyocheza. Nilikuwa nacheza sana rafu pia umbo langu lilikuwa dogo sana nashukuru baadae nilipewa mkataba kutokana na Ushauri wa mwalimu.

Aina Yake ya Uchezaji.
“Mimi napenda sana kucheza mpira wa nguvu. Mwanzoni nililaumiwa sana kwa uchezaji wangu. Na hii ndio sababu kubwa iliyofanya ninyimwe mkataba
.


Nakumbuka aina hii ya uchezaji wangu ilinifanya nimchukie mwamuzi mmoja tulipokuwa tunacheza daraja la pili. Wakati ule ulikuwa msimu wangu wa mwisho kabla sijaja Stand. Kwenye mchezo wa mahasimu wawili Kati ya Gulioni na Mlandege. Ulikuwa mchezo wa kukata na shoka. Mchezo wa kwanza tulipata ushindi wa goli 1 kwa 0 Ugenini. Niliporudi nyumbani mashabiki walitupokea kwa shangwe.

Niliwahakikishia kabla sijaondoka lazima timu yao ipande daraja la kwanza. Jitihada zake za kuipandisha timu daraja la kwanza ziligonga mwamba baada ya mwamuzi kumtoa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza faulo mbili na kutoka nje kwa kadi za njano mbili. Klabu yao ilipigwa magoli mawili kwa Moja na kutemwa katika hatua ya 4 bora.

Maisha yake Binafsi
Kama ilivyo kawaida mchezo wa soka umekuwa biashara nzuri kwa vijana waliotokea familia duni. Asilimia kubwa ya maisha yake ya soka yalisimamiwa na Kamal Manji ambaye pia alikuwa mmiliki wa klabu ya Mlandege. Wakati wa mchezo wa kwanza kati ya Mlandege na Gulioni Manji alilia sana lakini kwenye mchezo wa Marudiano ilkuwa zamu ya Ally kulia uwanjani.
Manji alikuwa akimhudumia kwa kiasi kikubwa kama vile nauli, viatu na jezi za mpira. Hawezi kabisa kumsahau. Anasema kwa sasa ana mchumba ambaye siku sio nyingi huenda akafunga nae pingu za maisha. Yeye ni mshabiki wa Rea Madrid na anampenda Sana Sergio Ramos.

Mchezaji aliyewahi kunisumbua sana ni John Bocco. Shida kubwa ilikuwa mwili wangu. Kila nilipojaribu kumsogelea alikuwa ananitoa njiani”

Timu ya taifa
Anasema kwenye kikosi cha Zanzibar alipigiwa simu na kaka yake kuwa ameitwa kikosini. Kwa bahati mbaya hakuweza kufika kutokana na majeraha. Ndoto yake kubwa ni kuvaa jezi za timu ya taifa Stars.

Kitu gani kinakukera sana?
“Tatizo kubwa la wachezaji wetu wa ndani hatujitumi na tunataka mafanikio ya haraka haraka. Wengine wakishapata hela wanazamia kwenye starehe na wanawake”

Takwimu
Mpaka sasa ana goli moja kwenye timu yake ya Stand United.

Ushauri wake?
Wakati najiunga Na Stand kila mtu alinidharau sana. Umbo langu dogo liliwafanya wengi wanidharau. Waliona sitoweza kuhimili vishindo. Nashukuru Mungu nimebadili yale mawazo potofu yaliyotawala akili za watu kuhusu uwezo wangu. Kikubwa jitume ili kubadilisha dhima mbaya kwa jamii juu yako”

Imeandaliwa na Priva Abiud
Instagram Privaldinho
Usisahau Kusubscribe Dauda TV

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here