Home Kitaifa Mambo matatu anayofanya Juma Mahadh kabla ya mechi

Mambo matatu anayofanya Juma Mahadh kabla ya mechi

7637
0
SHARE

Kila mtu ana utaratibu wake aliojiwekea kwenye maisha ya kila siku, kwa upande wa kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadh yeye ana utaratibu wake pia kabla ya kwenda uwanjani kutekeleza majukumu yake ya kazi.

Kabla ya kila mechi Mahadh hufanya mambo matatu ambayo ni muhimu kwake na anaamini yanamchango mkubwa kwake na kwa timu yake.

Mahadh amezungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ na kutaja vitu vitatu ambavyo huvifanya kabla ya mechi.

“Kabla sijaondoka hotelini lazima niombe Mungu kwanza, halafu namjulisha mama yangu kwamba naenda kwenye mechi aniombe baada ya hapo ni visingeli mwanzo mwisho.”

Unaweza ukajiuliza ni kwa nini anasikiliza muziki wa singeli na si aina nyingine ya muziki, mwenyewe amesema kwa sababu muziki huo huwa unaamsha mzuka.

“Singeli ni muziki wa kuamsha-amsha, sisi tunaenda kwenye mechi ambayo ni mchezo wa kuchangamka kwa hiyo inabidi upate kitu kitakacho kuchangamsha.”

Mwanzoni mwa mwaka huu aliandika waraka wa kuomba radhi kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga kuhusu kila kitu ambacho kilitokea nyuma na kuamua kuanza upya. Mkazuzu amemuuliza maendeleo yakoje tangu aamue kuanza upya.

“Namshukuru Mungu kila kitu kinaenda vizuri na nashukuru watu nilionao sasa hivi wananipa sapoti na hamasa kunifanya niwe najitihada zaidi kwa sababu naamini mwanzo nilikosea lakini nimeamua kujirekebisha na watu nilionao ninsahihi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here