Home Makala Kidato cha Sita wamemuona Ronaldo lakini?

Kidato cha Sita wamemuona Ronaldo lakini?

12289
0
SHARE

Sitaki niongelee ubora wa magoli yake. Sitaki nizungumzie suala la ushindani wake na Messi maana sio la msingi sana. Ronaldo ni mchezaji ambaye kidato cha sita wanapaswa kujifunza kupitia kwake. Kusoma ni kufanya mazoezi. Kucheza mechi ni sawa na kufanya mitihani.

Huenda Ronaldo ameonekana akijaribu kufanya baadhi ya mambo yanamshinda. Huenda wewe wakati unaanza shule umewahi kufeli n.k. Wakati Ronaldo anakuja United alikuwa anapiga sana mikasi anakosea. Alikuwa anapiga sana mashuti anakosea. Alikuwa anapenda sana chenga.

Usumbufu alioufanya Ronaldo makocha walimvumilia. Kuna kitu Ronaldo alikuwa anakosea. Alikuwa hajui wakati gani afanye nini. Huenda na nyie wanafunzi ambao najua wakati huu mpo nyumbani mnakula pasaka kuna wakati hamjui la kufanya na wakati gani. Tumekuwa tunasoma sana kipindi cha mitihan na tunataka tufanye vyema. Tumekuwa tunacheza sana wakati wa kusoma kisha wakati wa mitihani tunaanza kuhangaika.

Kidato cha sita mwezi wa 5 mnaenda kwenye mitihani. Naomba niwafundishe kitu. Mara kadhaa umefeli majaribio. Hata Ronaldo alikosea sana mikasi. Kuna wakati masomo yamekuwa magumu. Hata ronaldo juzi kwenye mechi ya Misri kuna chenga alikosea. Kuna mechi Moja ronaldo aliruka juu afunge kama Rooney akaukosa mpira.

Kukosea ni jadi yetu. Licha ya kwamba Ronaldo amekuwa anakosea lakini kila mara alipofanikiwa kuyafanya hayo ameleta kilio duniani. Kila wakati Ronaldo alipofanikiwa alihakikisha wanaomchukia wanalala kwa tabu. Ni wengi sana hawaamini uwezo wako kazini au darasani nakadhalika. Amini uwezo wako na hakikisha unasoma kwa bidii kabla hujaingia chumba cha mtihani kama Ronaldo anavyofanya kwenye kiwanja cha mazoezi. Usikubali kuabika kwenye chumba cha mitihani jiandae vyema ili ukiingia kwenye chumba uwe mtulivu kama Ronaldo uwanjani. Usiogope kukosea.

Ronaldo alizomewa na mashabiki wa Juventus. Dakika chache baadae ilibidi wamshangilie. Ronaldo alitimiza ahadi yake ya mazoezi. Kidato cha sita niwape siri moja ambayo inamfanya Ronaldo huu mzee azidi kuwaliza vijana. Kwanza Ronaldo uwanjani amepewa (Je wewe kwenye chumba cha mtihani unakuwaga na wenge?) Ronaldo hatumii tena chumba cha darasa kama sehemu ya kufanyia majaribio. Kidato cha sita tumekuwa na kasumba wakati wa kusoma hatusomi ila tunahangaika kwenye vyumba vya mtihani

Ronaldo amekuwa anatumia muda mwingi zaidi kwenye mazoezi. Ukimuona uwanjani anazurura tu mara kwa mara ila anajua anahifadhi mguvu zake na anajua alichokifanya kwenye mazoezi lazima akirudie. Vijana wa kidato cha sita hamsomii mnataka kuja kussumbua wengine kwenye chumba cha mitihani.

Angalieni Ronaldo anavyotulia uwanjani… haimaanishi amechoka.. nooo.. ila amejiandaa vyema kwenye mazoezi. Unasubiri nini wewe kidato cha 4? Kidato cha 6? Hata wale wa chuo. Jiandae vyema wakati wa kusoma ili ukiingia darasani urilaksi.

Ronaldo anajua vyema umri wake unamtupa mkono. Kidato cha sita mnajua wazi muda uliobaki ni mchache.

Ronaldo anachohitaji ni kuhakikisha kila shuti atakalopiga liwe na madhara. Na wewe hakikisha kila topiki utakayogusa likitoka swali hung’ai sharubu kama umebanwa na mlango. Hakikisha unakwenda chuo kikuu na wewe. Huenda chuo kikuu kwa Ronaldo ni kutwaa kiatu cha ufungaji bora au Ballon D Or. Kidato cha sita niwatakie kila la kheri.

Imeandaliwa na Priva Abiud
Instagram unaweza kunifollow Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here