Home Kitaifa Kuelekea Njombe Mji vs Simba “Kama kuna mechi ambazo sipendi nikiwa kocha...

Kuelekea Njombe Mji vs Simba “Kama kuna mechi ambazo sipendi nikiwa kocha ni kama hizi”-Masoud

7973
0
SHARE

Leo Aprili 3, 2018 ligi kuu Tanzania bara itaendelea kwa mchezo mmoja wa ‘kiporo’ unaozikutanisha Njombe Mji dhidi ya Simba. Mchezo huo utachezwa uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema mchezo huo utakuwa ni mgumu kwa sababu wanacheza dhidi ya timu ambayo inataka kujiokoa isishuke daraja wakati huo Simba inahitaji kuendelea kushinda ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda ubingwa wa VPL.

“Kama kuna mechi ambazo sipendi nikiwa kama kocha ni kama hizi, timu inayopambana kukwepa isishuke daraja na nyingine inawania ubingwa, mechi hizi zinakuwa ngumu sana lakini sisi ni timu kubwa tuna wachezaji wenye uzoefu wanajua nini wanataka uwanjani, tutapambana kama kawaida”- Masoud Djuma.

Kuhusu mkude Masoud amesema: “Wachezaji wote wako salama kabisa labda Mkude ambaye alipata majeraha lakini wengine wote wako vizuri tunashukuru kwa hilo.”

Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya magoli ikiwa sawa kwa pointi na yanga (zote zinapointi 46) lakini Yanga iko mbele kwa mchezo mmoja. Njombe Mji ina pointi 18 ikiwa nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here