Home Kimataifa Juventus Vs Real Madrid: Buffon afunguka kuhusu Ronaldo

Juventus Vs Real Madrid: Buffon afunguka kuhusu Ronaldo

11955
0
SHARE

Kuna maswali tata ambao Buffon anapaswa kuyajibu. Kwanza zimepita siku 300 baada ya kupata kipigo pale kwenye ya fainali mjini Cardiff. Umri wa Buffon ni Miaka 40, umri wake umeenda sana na ndoto zake ni kutwaa ubingwa wa uefa.

Buffon;
“hakuna maelezo zaidi juu ya mchezo huu, ila nataman sana kuanza kushinda katika michezo ya fainali. Tulipoteza tena kwenye fainali dhidi ya Barcelona, nina imani bado tunaweza kushinda ndani ya dakika 180 na pia tunaweza kupoteza kwenye dakika 90. Kwenye mchezo wa fainali tutahakikisha kuwa tutacheza kama tunapavyopaswa kucheza ndani ya dakika 180. Hakuna maelezo ya zaida kwani tuna uwezo na tumeshazoea kucheza michuano mikubwa kama hiyo. Timu hazichezi sawa kwenye dakika 180 kama inavyokuwa kwenye dakika 90”

Alipoulizwa kuwa wanapaswa kufanya nini ili kuifunga Real Madrid?

alisema

hilo ni jambo linalofanyika uwanjani na sio mdomoni, cha muhimu kujituma kwa kila tuwezalo, hicho ndicho mwalimu wetu anachohitaji tufanye”


PATA KIFURUSHI


Huu ni mchezo wa 20 kwa miamba hawa
Wa ulaya kukutana.
Madrid wameshinda mara 9
Juventus wameshinda mara 8

Madrid imeiingia fainali 16

Zidane atarudi tena katika mgahawa wake wa zamani aliozoea sana hapo awali kupata mlo pamoja na wachezaji wenzake kipindi akiwa klabuni hapo. Mgahawa huu unajulikana kama Restorante Da Angelino. Mmiliki wa mgahawa huu anasema anatamana sana kumuona Zidane anakuja tena kabla au baada ya mechi ndani ya mgahawa huo. Taarifa za timu

Juventus watakosa huduma za Kiungo Miralem Pjanic na Beki wao Medhi Benatia. Hata hivyo taarifa za ndani zinadai huenda beki wao wa pembeni Sandro Alex, Giorgio Chiellini, Sami Khedira wakawepo baada ya kuwa na majeruhi. Real Madrid hawana mchezaji yeyote aliyepo Majeruhi.
Ufanisi na maendeleo ya timu zote

Juventus wanaongoza ligi ya Italia wakiwa na alama 78 wakiwa tayari wamekwisha kufunga magoli 70 na kuruhusu magoli 16 pekee. Real Madrid wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 67 huku wakiwa wamefunga magoli 76 na kuruhusu magoli 33. Kwa uwiano huu ukiachilia mbali ukubwa na ubora wa ligi zote hizi. Juventus wanaonekana kuwa na takwimu bora zaidi hasa kwenye suala la ulinzi ukilinganisha na Real Madrid kwenye ngazi ya ligi.


Kwenye hatua ya Robo fainaili ya UEFA

Wote wamekutana na timu ngumu. Real Madrid imeitoa PSG miamba wa Ufaransa kwa idadi ya magoli matano kwa mawili, Juventus imefanikiwa kuitoa Tottenham kwa idadi magoli manne kwa matatu. Hivyo wote wamepita kwenye tanuru la moto kabla ya kufikia hatua hii.

Kwenye makundi wote walimaliza nafasi ya pili. Juventus akiwa nyuma ya Barcelona akiwa na magoli 11 akiwa amefunga magoli 7 na kuruhusu matano. Real Madrid walimaliza nyuma ya Tottehnam wakiwa na alama 13 ikiwa imefunga magoli 17 na kuruhusu magoli 7. Real Madrid hapa wanaonekana kuwa na ufanisi mkubwa kwenye ufungaji kuliko kuzia. Hili pia nalo ni tatizo lingine.
Itakuwaje

Safu ya ushambuliaji ya Juventus ni butu hasa katika michezo migumu. Safu ya ulinzi ya Real Madrid ni mbovu isipokuwa inabebwa na ufanisi wa Ronaldo.

Ni mchezo mgumu kwa Juventus maana jitihada zake zote watawekeza kwenye kuzuia. Hakuna kazi ngumu uwanjani kama kuzuia. Real Mardid watakachofanya ni kuhakikisha kuwa wanaweza kuipenya ngome ya Chielin. Kama Juventus wataruhusu kushambuliwa watakuwa wanampa Ronaldo nafasi kubwa zaidi ya kucheza kwa kujiamini uwanjani kwani safu yao ya kiungo itakuwa huru katika kushambulia zaidi kuliko kuzuia.

Sami Khedira, Stephan Lichtsteiner, Giorgio Chiellini and Gonzalo Higuain

Safu ya ushambuliaji ya Juventus kwenye michezo migumu. Kwa mfano katika michezo yake migumu ya mwisho hawajaweza kufunga zaidi ya magoli.

Juventus 0-0 Inter Milan
Napoli 0-1 Juventus
Juventus 1-2 lazio
Juventus 1-0 Roma


Kauli ya Buffon kwa Ronaldo inaleta picha tofauti. Buffon anasema kuwa Amewahi kucheza na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa mashuti kama David Trazeguet na Zlatan Ibrahimovic lakini anasema Ronaldo ni mchezaji aliyekamilika zaidi kwenye uwezo wa mashuti. Inaonekana wazi kuwa Buffon licha ya kuwa na uwezo mkubwa golini lakin bado anaogopa mashuti langoni kwake.

Wachezaji wa kutazamiwa

Cristiano Ronaldo ana magoli 37 kwenye michezo 35. Amechangia magoli 12 na amechangia magoli 22 katika michuano ya uefa. Ni mchezaji hatari zaidi duniani kwa sasa. Macho ya watailiano yote yataelekezwa kwake.
Gonzalo Higuain

Hajawa na msimu mzuri sana katika timu yake ya taifa lakini kwenye klabu yake ni mchezaji wa kutegemea. Kwenye michuano ya UEFA amefunga magoli matano. Amekuwa akishirikiana vyema na Paul Dybala. Ni mchezaj wa Zaman wa Real Madrid. Atahitaji kufanya vyema ili kumtambia Ronaldo
Paulo Dybala

Amekwisha funga magoli 18 na kutengeneza magoli 4. Kiujumla amekuwa msaada mkubwa kwenye timu. Dybala ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Argentine na huu ni wakati muafaka wa yeye kuonesha kuwa ndiye mchezaji anayepaswa kucheza katika kikosi cha Sampaoli.
Buffon

Tayari amekwisha weka hofu yake kubwa kwa Ronaldo lakini huyu ni moja ya makipa wagumu na wenye heshima zao kabisa.

Vita itakuwa wapi?

 


Ronaldo Vs Chielin
Dybala Vs Ramos
Casamero Vs Khedira

imeandaliwa na Priva ABIUD, unaweza kunfollow Instagram @Privaldinho

usisahau kusubscribe youtube Channel ya Dauda TV.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here