Home Kimataifa Bayern Munich ni mlima mrefu kwa Sevilla, wataweza kuupanda hii leo?

Bayern Munich ni mlima mrefu kwa Sevilla, wataweza kuupanda hii leo?

7122
0
SHARE

Hakuna aliyetarajia kwamba Sevilla wangeitoa Mancheter United kama sasa hivi ambavyo kila mtu anaipa nafasi Bayern Munich kusonga mbele, na hii leo Sevilla wanawakaribisha Bayern nyumbani kwao Ramon Sanchez-Pizjuan.

Kocha wa Sevilla Vincenzo Montella anaona uwezekano wa Sevilla kuitoa Bayern Munich na ameahidi wachezaji wake watajitoa zaidi na watapambana kwa kila hali ili kuiondoa Bayern Munich katika michuano hiyo.

Bayern Munich wanakwenda katika michuano hii wakiwa wametoka kutoa onyo kali kwa wapinzani wao baada ya kuwachapa Borussia Dortmund mabao 6 kwa nunge mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ever Banega kiungo wa Sevilla ambaye amecheza michezo yote ya Sevilla msimu hiu hatakuwepo hii leo kutokana na kutumikia adhabu, huku Sebastian Crochia akiwa bado ana majeruhi.
Kwa upande wa Bayern Munich Manuel Neuer bado ataendelea kukosa mchezo huo kutokana na majeruhi, Kingsley Coman naye hivyo hivyo hatakuwepo katika mchezo wa leo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Bayern Munich wana rekodi mbovu dhidi ya vilabu vya kutoka nchini Hispania katika hatua kama hii, mechi zao zote walizocheza na Wahispania katika michuano 4 iliyopita waliondolewa.

Ni timu mbili ambazo zina rekodi mbili tofauti katika timu 8 zilizobaki katika masuala ya mashuti, kwani Sevilla ndio timu iliyobaki yenye mashuti machache( wastani wa 10.1%) huku Bayern Munich ndio wana rekodi nzuri ya mashutu (12.7%).

Sevilla hawajawahi kucheza michezo 6 barani Ulaya bila kupoteza mchezo hata mmoja, na hadi sasa wana michezo 5 bila kupoteza. Katika mechi zao 5 zilizopita Juventus wameshinda mechi 2 na kusuluhu michezo 3.

Tishio kubwa sana kwa Sevilla hii leo ni Robert Lewandowski ambaye katika michezo 28 ya Champions League hadi sasa amefunga mabao 22 tangu 2015/2016 huku wiki iliyopita akitoka kufunga hattrick dhidi ya BVB.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here