Hivi majuzi kuna kijana mmoja alinitafuta akanielezea baadhi ya changamoto ambazo amekutana nazo hivi karibuni. Anaitwa Dominicusius Kuhanga, ana umri wa miaka 17. Kwa bahati mbaya sana sijamuona akicheza. Kwa kuwa sijamuona haimanishi kuwa nisimuongelee.
Kimsingi huyu jamaa anachezea kule Zimbabwe. Ni mtanzania anacheza klabu ya Aces youth soccer academy huko huko nchini Zimbabwe. Kwa maelezo yake na ya kocha wake na historia yake inaonesha ni mchezaji mwenye kipaji na mwenye shauku na ndoto za kuitumikia Tanzania katika ngazi zote. Anasema kuna tatizo katika kufikia daraja hilo.
anasema hivi nanukuu, “Bro nimekuwa nikipambana sana kuhusu ndoto yangu katika akademi hii na ninazidi kuimarika kila siku,,,,,, shida yangu ni kuhusu U-20 ya timu ya taifa,, Bro, nimekuwa nikihangaika kuwatafuta viongozi wengi wa TFF na kuwatumia taarifa zangu na kuomba kujumuishwa katika timu ya taifa ya vijana ili nifanye majaribio lakini mara zote wamekuwa wakikaa kimya tu, hakuna hata majibu, sasa mimi siwaelewi yaani kwanini hawatoi nafasi hizo au hata kusema hapana hakuna nafasi”
KUHANGA amezaliwa 27 Nov 2000.
Amezaliwa na kukulia TABORA, TANZANIA
Vilabu vya hapo awali
KAISERS FC (Tabora 2012-14)
CHIPUKIZI ACADEMY ( Tabora 2014)
MARA SPORTS ACADEMY (musoma 2015-2017)
Pia aliiwakilisha Tabora katika mashindano ya Copa coca Cola U-15 mwaka 2013 na 2014
Nilipomuuliza kuhusu safari yake ya Zimbabwe ilikuwaje alisema,
Nikajaribu kumuuliza kama aliwahi kufanya mawasiliano na wahusika wa hapa tanzania akanijibu “Ndioooo,,,,,, niliwasiliana na mwalimu Bundala (trainee wa makocha TFF) Pia nimeshatuma sana email zangu kwenye Email ya TFF bila majibu, Nikamtafuta kocha Kenny Mwaisabula ila akaniahidi atashughulikia lakini tangu hapo hajibu meseji zangu kabisa” (kuhusu taarifa hizi za kuwasiliana na Kenny mwaisabula hatujathibitisha maana sijafanikiwa kumpata hewani)
Kwa maelezo yake ni kiungo wa katikati. Klabu yake kwa sasa inashiriki ligi ya taifa ya U-21 na pia wamefika hatua ya fainali ya kombe Zimbabwe Challenge league inayotarajiwa kuchezwa wiki hii.
Najua wapo vijana wengi mtaani wenye uwezo. Sio huyu tu. Wapo wengi mtaani. Tumekuwa na timu mbovu kwa kuwa tunaitana kwa kujuana. Wapeni nafasi vijana wafanye majaribio. Msiwapuuze kabla hamjawajaribu. Mchezaji yoyote akija msikilizeni mpen mpira mtaona tu kati ya tui la nazi na maziwa. Narudia tena huyu kijana simjui lakini najua hizi ni changamoto ambazo zipo. Namba zake ninazo, kwa mwenye mawasiliano na msaada wowote anitafute nitakuunganisheni nae nitafute kwenye 0763370020
Imeandaliwa na Priva (unaweza kunifollow Instagram kwa jina la Privaldinho)
Na usisahau kusbscribe Youtube channel ya Dauda Tv.