Home Dauda TV Video-Povu la Ammy Ninje baada ya kubanwa na wandishi wa habari

Video-Povu la Ammy Ninje baada ya kubanwa na wandishi wa habari

13866
0
SHARE

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 20 Ammy Ninje alishindwa kuzuia hasira zake mbele ya waandishi baada ya kuulizwa kwa nini hakuwatumia baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakipewa nafasi kwenye klabu za ligi kuu.

Ninje alijikuta ‘akikoromeana’ na mwandishi aliyeuliza swali hilo kwa kumwambia aulize maswali yake kuhusu wachezaji ambao walicheza.

Jana Jumamosi Machi 31, 2018 Ngorongoro Heroes ilicheza dhidi ya DR Congo mchezo wa kuwania kucheza fainali za Afrika kwa vijana wa U20 na kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wa taifa.

“Unafanya makosa sana kuzungumzia wachezaji ambao hawajacheza wakati kunawachezaji 11 wamecheza, zungumzia wachezaji waliocheza usizungumzie majina unayoyataka wewe ya Yanga, Lipuli na mengine, sipendi”-Ammy Ninje

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here