Home Kimataifa Mara ya mwisho Spurs kupata ushindi Stamford Bridge sikuwa nimezaliwa, leo wataondoa...

Mara ya mwisho Spurs kupata ushindi Stamford Bridge sikuwa nimezaliwa, leo wataondoa nuksi?

7327
0
SHARE

Je wajua? Tottenham Hotspur wana michezo 25 ya Epl katika uwanja wa Stamford Bridge bila ushindi, hii ni rekodi katika EPL kwa timu moja kucheza katika uwanja mmoja wa wapinzani mechi nyingi bila ushindi.

February mwaka 1990 wakati Tottenham wakiifunga Chelsea mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani ilikuwa mara ya mwisho kwa Spurs kuifunga Chelsea katika uwanja huo na michezo 30 iliyofuata katika mashindano tofauti, Spurs hakupata ushindi.

Katika michezo yao miwili iliyopita vs Chelsea katika uwanja wa Chelsea, Tottenham walitangulia kupata bao lakini zote wakashindwa kupata ushindi, May 2016 walitangulia 2-0 mechi ikaisha 2-2, iliyofuata walitangulia 1-0 mechi ikaisha wamepigwa 2-1.

Lakini uwezo wa Chelsea katika siku za hivi karibuni umekuwa ukitia mashaka sana, katika mechi zao 6 za mwisho wamepetoza michezo 4 huku mechi 2 zilizobaki wakiwa wameshinda na leo wakishinda watakuwa wameshinda mechi 2 mfululizo.

Michezo 4 ya Chelsea dhidi ya timu ambazo ziko top 6 Chelsea wameshindwa kupata ushindi, wamepoteza 2 na kusuluhu 2, na wameshinda mechi 2 tu kati ya 8 za mwisho dhidi ya timu ambazo ziko top 6 EPL.

Spurs wanashikilia rekodi ya kutofungwa mchezo hata mmoja wa EPL mwaka 2018 wakiwa wameshinda 7 na kutoka suluhu michezo 3 huku wakiwa wameshinda michezo yao 4 ya mwisho na kuruhusu wavu wao kuguswa mara moja tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here