Home Kimataifa Huu ni ushindi wa kwanza kwa Spurs tangu 1990, lakini na haya...

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Spurs tangu 1990, lakini na haya unayafahamu?

10383
0
SHARE

Huu ulikuwa ushindi wa kwanza wa Tottenham katika uwanja wa Stamford Bridge tangu 1990, ilikuwa mwezi February mwaka 1990 wakati Tottenham wakiifunga Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani.

Bao la kuongoza la Chelsea liliwekwa kiamiani la Alvaro Morata kwa kichwa na hili likiwa bao lake la 7 la kichwa msimu huu (anaongoza kwa mabao ya kichwa) na bao la 14 la Chelsea la kichwa msimu huu(ndio klabu inayoongoza kwa mabao ya kichwa).
Tot walisawazisha bao hilo kupitia kwa Christian Erriksen ambaye sasa anakuwa mchezaji wa 3 wa Spurs kufunga bao zaidi ya moja uwanjani kwa Chelsea ambapo anaungana na Teddy Sheringham(3) na Fredi Kanoute(2).

Baada ya kipindi cha pili kuingia Dele Alli alifunga mabao mawili kwa Tottenham (62,66) yalioumaliza mchezo kwa Tot kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-1 na kuifanya Chelsea kupoteza michezo 5/7 ya mwisho EPL.

Kwa sasa Tottenham wanakuwa wamecheza jumla ya michezo 13 bila kupoteza mchezo hata mmoja wa ligi huku michezo yao 5 ya mwisho katika EPL wakiwa wameshinda yote na kuifikia rekodi ya Man City ya ushindi wa mechi 5 mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here