Home Kimataifa Ujasusi wa Urusi waliweka rehani kombe la dunia, UK na US waungana...

Ujasusi wa Urusi waliweka rehani kombe la dunia, UK na US waungana dhidi yao

12147
0
SHARE

Kuna tukio linaendelea kuleta mvutano wa chini chini kati ya Urusi na taifa la Uingereza, mvutano huu ni wa kidiplomasia ambapo Waingereza wamekuwa wakiishutumu Urusi kwa jaribio la mauaji ya raia wao wawili.

Sergei Skripai na mtoto wake wa kike aitwae Yulia wanadaiwa kupewa sumu nchini Urusi mwezi jana, sababu kubwa kwa Skripai kupewa sumu ilikuwa ni kile kinachodaiwa kwamba Skripai alikuwa shushushu wa Uingereza aliyetumwa nchini Urusi.

Tangu  Skripai na binti yake wapewe sumu Uingereza wamekuwa wakidai hatua kubwa zichukuliwe dhidi ya Urusi kwa tukio hilo huku nao wakitishia kuacha kuuza bidhaa za Urusi katika nchi ya London.

Kuna wakati waziri wa mambo ya ndani ya Uingereza ameliihusisha michuano hii na michuano ya Olympic mwaka 1936 nchini Ujerumani wakati wa vita baridi, akimaanisha kwamba kombe hili linafanyika katika mazingira kama ya Adolf Hitler na utawala wa kikatili wa Nazi.

Moja ya mbunge wa chama cha upinzani nchini Uingereza ameshauri kwamba kutokana na suala hili kutokuwa na ufumbuzi baasi ni vyema michuano hii ikasogezwa mbele ama kufutwa kabisa kwa mwaka huu.

Wakati Uingereza wakicharuka kuhusiana na tukio hilo, Marekani nao wanaonekana kuingilia kati jambo hilo hali iliyopelekea Wanadiplomasia 170 wa Urusi kuondoka nchini Marekani pamoja na familia zao na kurudi Urusi.

Huko Urusi nako katika jiji la St Petersburg inadaiwa kwamba serikali ya Urusi imeamuru kushushwa kwa bendera ya Marekani katika ubalozi wao ulioko katika mji huo.

Waziri wa mambo nje wa Urusi Maria Zakharova ameongea na Channel 5 Tv ya nchini Urusi na katika mahojiano yake amezishutumu US na UK kwamba hawana lolote bali wanachotaka ni kuvuruga michuano hiyo.

Bado hali ya Skripai ni mbaya na hadi sasa hajitambui huku hali ya binti yake ikitajwa kuanza kuimarika taratibu na kuanza kuongea taratibu na hakuna taarifa yoyote kutoka timu ya taifa ya Uingereza hadi sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here