Home Kimataifa Anthony Joshua aibuka kidedea kama kawaida, sasa amtaka Wilder

Anthony Joshua aibuka kidedea kama kawaida, sasa amtaka Wilder

7347
0
SHARE

Baaada ya tambo za muda mrefu hatimaye bondia wa Uingereza Anthony Joshua amempiga mpinzani wake kutoka New Zealand Joseph Parker na kutwaa ubingwa wa IBF, WBA, IBO na WBO.

Joshua alishinda mchezo wa leo usiku kwa point ambapo majudge wawili walitoa point 118-110 huku judge mmoja akitoa point 119-109 point ambazo zilimpa Joshua ushindi katika mechi hiyo iliyofanyika Cardif.

Parker hakuwa mbaya sana lakini mda mwingi kambi yake ilionekana kulalamika sana haswa katika raundi ya nne baada ya kuona kama bondia wao anachezewa faulo wakati alikuwa amezidiwa sana na Joshua.

Baada ya pambano la Joshua aliulizwa swali ambalo kila mpenda masumbwi alitamani aulizwe kuhusu pambano lake na Deontay Wilder na Joshua aliwajibu walichotaka kusikia kwa kuwaambia pambano hilo lina uwezekano wa kuwepo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here