Home Kimataifa “Washtue wana wakawashtue wana” kwamba zimebaki siku 9 twende Escape One

“Washtue wana wakawashtue wana” kwamba zimebaki siku 9 twende Escape One

5552
0
SHARE

Bado michezo 8 tu kwa msimu huu wa EPL kufungwa, na kwa baadhi ya timu kama Liverpool kwao zimebaki mechi 7 tu ili kuweza kufunga msimu huu wa ligi ambao tayari bingwa ameanza kuonekana.

Pep Gurdiola anaonekana kutaka kubeba ndoo yake ya kwanza ya EPL katika maisha yake ya soka, na hakuna jambo la kuvutia kama Pep kubeba ndoo hii kwa kuwapiga mara mbili mfululizo wapinzani wake wakubwa Manchester United.

Lakini sio kazi rahisi kwa kocha aina ya Jose Mourinho kukubali kupigwa mara mbili mfululizo na mpinzani huyo huyo na hii inaifanya Manchester Derby kuwa mechi ngumu sana tofauti na mwanzo.

Kwa nini nimeiongelea Derby hii moja kwa moja na kuachana na michezo ya wiki hii? Nimeizungumzia Derby hii kwa sababu tarehe 7 April siku ya mchezo huu mashabiki wote wa timu hizi watakutana Escape One pale mikocheni kuangalia derby mbili kubwa nchini Uingereza.

Siku hii hii ambayo inaonekana kama sikukuu kwa wapenda soka kutakuwa na Merseyside Derby, Liverpool watakuwa nyumbani kuwakaribisha wapinzani wao wakubwa katika michuano ya EPL klabu ya Everton, na hii pia tutaiangalia kwa pamoja Escape One.

Siku hii inaweza kuwa siku kubwa zaidi EPL katika siku zilizobaki na ndio sababu “Washtue Wana wakawashtue wana” tukaangalie pamoja michezo hii tarehe 7, tutakuletea tathmini na takwimu muhimu kuhusiana na mechi hizi katika siku 9 zilizobaki kuelekea Escape One.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here