Home World Cup Road 2 Russia: Denmark watashangaza Wengi kule Russia

Road 2 Russia: Denmark watashangaza Wengi kule Russia

7409
0
SHARE

Tiketi ya Bombardier

Denmark ni nchi ndogo tu. Ina watu kama milioni 6 hivi. Ni taifa dogo sana kule ukanda wa Scandinavia. Wamekuwa na timu ya taifa nzuri ambayo kwa bahati mbaya haina jina kubwa sana. Mwaka huu wapo kundi C pamoja na mataifa ya France, Peru na Australia. Denmark anakutana na mbabe wake wa mwaka 1998. Kuna baadhi ya vipaji murua kabisa katika taifa hili ya Denmark. Denamrk wanaweza kufanya vyema kuliko timu zingine ambazo zinatazamwa zaidi kwa mambo yafuatayo.

Historia ya taifa hilo

Mwaka 1992 kikosi cha bwana Richard Moller Nielsen kiliishangaza dunia, kwa kuichabanga Ujeruman waliokuwa mabingwa wa kombe la dunia kwenye michuano ya Euro. Denmark walikuwa wakiongozwa na mlinda mlango anayeaminika kuwa mlinda mlango bora kuwahi kutokea Bwana Peter Schmeichel. Hicho ndicho kilikuwa kizazi bora kwa Denmark kwa wakati ule na katika Historia ya nchi hiyo.

Katika historia ya taifa ile hatuwezi kuacha kumzungumzia Brian Laudrup ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Denmark kwa mara nne na pia aliwahi kutajwa na FIFA mwaka 1992 kuwa mchezaji wa tano kwa ubora duniani kwa mwaka ule. Ni mchezaji ambaye simba wa soka kutoka Brazil Pele alimtaja katika orodha yake kuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora dunian kuwahi kutokea duniani akimweka nafasi ya 125.

Michael laudrupp ni kaka yake na Brian Laudrup. Wote hao wanatajwa kama wachezaji bora kukumbukwa katika ardhi ya Denmark. Michael Laudrap alifanikiwa na Barcelona Ajax Real Madrid na Juventus. Aling’ara sana chini ya Johan Cruyff. Alitwaa vikombe tisa ndani ya klabu ya Barcelona. Mwaka 1999 alitajwa kuwa mchezaji bora wa kigeni la liga kwa kipindi cha miaka 25.

Mwaka 2006 alitajwa na chama cha soka cha nchini humo kuwa mchezaji bora wa Muda wote kutoka Denmark. Wakati Laudrup mkubwa akitajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika nchi za Scandinavia. Anatajwa pia kuwa kati ya wachezaji 11 bora kigeni katika historia ya Real Madrid.

Wachezaji wenye uzoefu mkubwa

Tayari Andreas Christensen amekwisha cheza ligi kubwa mbili. Tayari ameshafanikiwa kupata nafasi katika klabu ya Chelsea. Sio jina geni sana. Anaweza kuwa mgeni kombe la dunia lakini sio mgeni kwenye mechi kubwa. Yupo Golikipa Imara kabisa Kasper Schemeichel. Ameshatwaa ubingwa wa Uingereza na ni moja ya magolikipa imara.

Yupo kiungo hatari wa klabu ya Tottenham Ericksen ambaye anawatoa udenda klabu ya Barcelona. Pia yupo mshambuliaji wa Zamani wa Arsenal Nicklas Bendtnar. Huenda asiwe mchezaji mzuri sana lakini uzoefu wake ni msaada tosha.

Nyota zinazong’aa

Tukiachana na kundi la akina Ericksen pia wapo vijana wadogo wanatoa mwanga gizani.

Pione Sisto. Mashabiki wa Man Utd watamkumbuka vyema kwenye mchezo wao dhidi ya Celta Vigo. Ni kiungo wa katikati hivi, mweusi, anakata mbuga kama N’golo Kante vile. Huenda wadernmark wasimsahau Michael Laudrup lakini huyu nae atafanya vyema. Akiwa na miaka 18 alikipiga katika klabu ya Midjytlland na alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka akiwa na miaka 18 tu. Shisto ana asili ya Uganda.

Pia yupo mshambuliaji wa Ajax Kasper Dolberg. Ndani ya Ligi kuu uholanzi tayari ameshafunga magoli 20 latika michezo 45. Viktor Fischer Pia yupo kiungo wa zaman wa Ajax ajulikanae kama Viktor Fischer mwenye miaka 23 ambaye aliichezea Ajax Michezo 80 na kufunga magoli 25 huku akiwa na magoli matatu timu ya taifa kwenye michezo 13 alitajwa kuwa mchezaji chipukizi mara mbili akiwa Denmark na baadae akiwa Ajax.

Pia akiwa kwenye michuano ya wachezaji wa chini ya miaka 17 aliweza kuifungia timu yake ya taifa magoli 20 katika michezo 30 na waliweza kufika nusu fainali ya kombe hilo kabla ya kufungwa na Ujeruman. Babu yake fischer pia alikuwa mcheza soka wa zaman wa taifa hilo bwana Poul Pedersen.

Imeandaliwa na Priva Abiud

Instagram Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here