Home Kimataifa INASIKITISHA: Atamani kujiua baada ya ndoto ya kucheza mpira kufa kwa upofu

INASIKITISHA: Atamani kujiua baada ya ndoto ya kucheza mpira kufa kwa upofu

10832
0
SHARE
Femi Opabunmi alikuwa na umri wa miaka 17 alipocheza dhidi ya England na David Beckham kwenye Kombe la Dunia la mwaka 2002

Femi Opabunmi aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuiwakilisha Nigeria kwenye michuano ya Kombe la Dunia alipocheza mechi dhidi ya England mwaka 2002. Miaka minne baadaye ndoto zake za kucheza soka zilikufa kutokana na tatizo la jicho hadi kufikia hatua ya kutaka kujiua.

“Nilikuwa na umri wa miaka 17 nilipoicheza Nigeria kwenye Kombe la Dunia mwaka 2002-mchezaji mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huo. Nilicheza dhidi ya England ya akina David Beckham, Michael Owen, Paul Scholes, wote hao. Lakini miaka mitatu au minne baadaye story ilibadilika, sekunde moja upo juu sekunde nyingine upo chini.

Tatizo langu la jicho ndipo lilipoanza. Ilibidi nifanyiwe upasuaji. Walisema nina tatizo la glaucoma. Kila kitu kilibadilika. Mambo yakawa mabaya zaidi na zaidi. Kwa sasa naona kwa jicho moja.

Siku moja niliamka asubuhi na kujikuta sioni vizuri. Nilikuwa naona ukungu ikanibidi kwenda kwa mtaalam kwa ajili ya uchunguzi. Ndipo niliambiwa inabidi nifanyiwe upasuaji. Baada ya upasuaji, tatizo lilibaki vilevile.

Sasa ninaona kwa jicho la kushoto. Sioni chochote kwa jicho la upande wa kulia. Namshukuru Mungu bado ninaweza kuona kwa jicho moja.

Kuachana na soka ni kitu ambacho kinaniuma sana. Wakati mwingine unawaza hata kujiua mwenyewe. Unafikiri kupita maelezo, hasa pale wachezaji wenzako wanapokuwa wanaendelea kucheza. Unawatazama na unaishia kulia. Unajisikia vibaya. Lakini katika kila hali inakubidi kuwa mvumilivu.

“Maisha ni kupanda na kushuka.

Nigeria haikufanikiwa kuvuka hatua ya makundi katika Kombe la Dunia mwaka 2002, ilimaliza ya mwisho kwenye kundi lilokuwa na timu za Sweden, England na Argentina

Nafikiria siku za nyuma, nafikiri sana kuhusu nilivyokuwa nashika nafasi ya pili kwa ufungaji katika mashindano ya U17 World Championship mwaka 2001 huku nikiwa mchezaji bora namba tatu. Nilikuwa mchezaji mdogo zaidi nilipocheza michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Korea Kusini na Japan.

Wakati mwingine nafikiria: “Haya maisha ni nini?” Naishia kujifariji kwa kusema: “Kwa sababu bado nipo hai, sikumoja kutakuwa na matumaini.”

Naweka matumaini yangu kwa Mungu. Naendelea na safari. Hakuna cha kufanya.

Kuna wakati najisemea: “Si dhani kama kuna Mungu duniani.” Lakini mke wangu ananifariji na kuniambia nisiseme maneno mabaya kuhusu Mungu, kwa sababu Mungu anajua muda muafaka na anamjibu kila mmoja. Huenda Mungu alikulinda na hatari, huwezi jua.

Kinachoniumiza zaidi ni katika kipindi hiki cha changamoto ni kwamba sikucheza mpira wakati nikiwa bado nadai. Ni jambo linaloumiza.

Nimejifunza sana kuhusu somo la hakuna aijuae kesho. Unaweza sema utacheza mchezo fulani kwa muda mrefu lakini kuna kitu kinatokea na kufupisha career yako.

Nilitengeneza pesa nyingi lakini ni hizohizo nilizitumia kwa ajili ya matibabu ya jicho langu. Ninachoweza kuwaambia wachezaji vijana wanaochipukia kwamba wafanye vyovyote lakini wanatakiwa kufikiri kuhusu kesho yao.

Wanatakiwa kuwekeza, wachukue story yangu kama mfano, wajifunze.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here