Home Kimataifa Hispania vs Argentina, nani wa kwanza kupata ushindi wa 4?

Hispania vs Argentina, nani wa kwanza kupata ushindi wa 4?

6580
0
SHARE

Wahispania wengi haswa kutoka Catalunya wanamchukulia Lionel Messi kama mtu wa kwao, kutokana na historia yake katika soka ambapo anaonekana maisha yake yote ya klabu ametumikia klabu kutoka Hispania (Barcelona).

Hakuna uhakika wa Messi kuwepo uwanjani hii leo wakati Argentina wakiikabili Hispania kwani hakuwepo dhidi ya Italia kutokana na mejeruhi na mwalimu George Sampaoli bado hajathibitisha kama L Pulga atakuwepo uwanjani hii leo.

Mechi baina ya timu hizi mbili mara zote imekuwa kati ya mechi ngumu sana na ambayo mara zote imekuwa haikosi mshindi na rekodi zinaonesha kwamba katika michezo 6 ya mwiso kati ya timu hizi mbili hapakuwa na suluhu.

Michezo yao sita ya mwisho wamekuwa wakigawana ushindi kwani Argentina wameshinda michezo mitatu kati ya hiyo sita huku Hispania nao wakishinda michezo mitatu kati ya sita huku hata mechi zao mbili za mwisho kila mmoja akishinda moja.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here