Home Kimataifa Ukarimu wa Barcelona huu hapa

Ukarimu wa Barcelona huu hapa

7477
0
SHARE

 

Barcelona ni moja ya klabu ambayo imekuwa na ukarimu kwa wakufunzi wake. Mara kadhaa baadhi ya walimu waliokwisha ifundisha klabu hii wamerudi tena kwa mara ya pili au zaidi kuifundisha timu hiyo. Ifuatayo ni orodha ya waalimu amabo waliwahi kufundisha klabu hiyo wakaondoka na kisha baadae kurudi tena,

John Richard Greenwell (1912-1917, 1931-1932)

Ni moja ya makocha walioifundisha Barcelona kwa kipindi kirefu zaidi. Aliifundisha klabu hiyo kwa miaka 7 kisha rekodi hiyo ikavunjwa na Yohan Cruyff. Pia aliwahi kuwa mchezaji wa Barcelona kutokea mwaka 1912 mpaka mwaka 1917.

Raisi wa Barcelona Bw. Joan Gamper alimteua kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 33 tu. Aliitumikia Barcelona mnamo mwaka 1917 mpaka 1923. Kisha alipoondoka alirudi tena mwaka 1931 na akaiongoza klabu kwa miaka miwili.

Richard Kohn (1926-1927, 1933-1934)

Ni myahudi pekee aliyeifundisha Barcelona miaka 1926 mpaka 1927. Alirudi tena mwaka 1933 mpaka 1934. Kabla ya kurudi alikuwa mwalimu mkuu wa klabu ya Bayern Munichen.

Alikumbwa na sekeseka la vita ya chama cha NAZI, dhidi ya wayahudi. Kutokana na vurumai hilo alikimbia nchini Ujerumani mwaka 1933. Hata hivyo akiwa nchini Ujerumani licha ya ubaguzi mkubwa wa NAZI bado aliweza kutwaa ubingwa wa Ujerumani mwaka 1932, ndiposa akatimkia Barcelona.

Ferenc Plattko (1934-1995, 1955-1956)

Huyu Alianza kibarua chake Kule katalunya mwaka 1934-1995 na alirudi tena mwaka 1955-1956. Huyu pia aliwahi kuichezea Barcelona mwaka 1923-1930. Alianzia safari yake ya soka mjini Budapest akicheza nafasi ya golikipa.

Rapahel Albert aliwahi kumwandikia mashairi mlinda lango huyu kwa kiwango bora alichoonesha pale Cam Nou. Kipindi hicho alicheza sambamba na nguli wa zamani Luis Suarez pamoja na mchezaji mtukutu kubala

Helenio Herrera (1958-1960, 1979-1980)

Ulishawahi kusikia ile Inter Milan iliyojulikana kama Grande Inter? huyu ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo wakati huo ulipokuwa tishio kubwa sana kule serie A. anatajwa moja ya makocha wakubwa duniani hasa kwenye michuano ya klabu bingwa tokea kuanzishwa kwa kombe la UEFA mwaka 1954. Alitwaa makombe mawili ya ulaya akiwa na Inter Milan, akatwaa Laliga mara 4, akiwa na Barcelona na Atletico.

Aliiongoza Barcelona mwaka 1958-1960. Akiwa Barcelona aligombana na mchezaji nguli wa klabu hiyo Ladislao Kubala kisha akatimikia Inter Milan. Alipotua Milan alitwaa makombe mawili ya ulaya, akaanzisha mfumo maarufu zaidi dunia wa Cattenaccio. Alirudi tena katalunya mwaka 1979 hadi mwaka 1980.

Ladislau Kubala (1963-1965, 1980-1982)

Huyu ndiye sababu kubwa ya Herrera kuondoka Barcelona. Mwaka 1949 nchi yake ya Hungary iliingia kwenye machafuko ambapo alikimbilia marekani na kuishi huko kama mkimbizi. Mwaka mmoja baadae alijiunga Barcelona ingawa hakuruhusiwa kucheza mpaka 1951. Baadae akina Luis Suarez na Evearisto walijiunga nae Barcelona mwaka 1958

Ugomvi wake na Herrera ulimfanya kukosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid mwaka 1960. Mwaka 1961 alistaafu soka na kujiunga na benchi la ufundi la Barcelona na kuwa kocha mkuu wa Barcelona mwaka 1963. Alitimuliwa miaka miwili na baadae. Mambo yalimwendea vizuri alipopata tena kandarasi klabuni hapo mwaka 1980 mpaka 1982.

Loius van Gaal (1997-2000, 2002-2003)

Wengi wanapenda kumtania mzee wa falsafa. Mwaka 1997 alitwaa nafasi ya Kocha Bobby Robson. Alinyakua makombe mawili ya la liga na kombe moja la Copa de la Rey. klabuni hapo anadai alikumbwa na changamoto nyingi ikiwepo mgongano wa yeye na mchezaji maarufu kutoka Brazil Rivaldo.

Mnamo mwaka 2000 aliondoka klabuni hapo na kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Uholanzi. Raisi wa Barcelona Gaspart ambaye pia alikuwepo wakati Van Gaal anaondoka klabuni hapo alimkaribisha tena van Gaal. Wakati huu mambo hayakuwa mazuri kabisa kwa Van Gaal kwa sababu alitimuliwa klabuni hapo ikiwa na tofauti ya alama 3 na klabu zilizokuwa hatarini kushuka daraja.

Imeandaliwa na Priva Abiud

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here