Home Ligi EPL Shaffih Dauda anavyomkingia kifua Sanchez Manchester United

Shaffih Dauda anavyomkingia kifua Sanchez Manchester United

10567
0
SHARE

Alexis Sanchez wa Manchester United ni tofauti kabisa na yule wa Arsenal,  tangu amejiunga na united bado watu wanasubiri hadi leo kushuhudia kiwango kilichomfanya mourinho akaamua kupambana kuipata saini yake katika kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Kushindwa kuonesha makali yake uwanjani kama ilivyotarajiwa kumezua mijadala mingi kwenye mitandano ya kijamii hadi kwenye vijiwe vya kahawa miajada mikali imekuwa ikiendelea juu yake, kwa sababu nafasi ya kucheza anapata sasa shida ni nini?

Shaffih Dauda ameibuka kumtetea Sanchez kwa kutoa sababu kadhaa ambazo anadai ndio zinafanya raia huyo wa Chile anaonekana si lolote si chochote siku za karibuni.

“Ukienda kuishi kwenye eneo jingine na kukutana na familia nyingine, katika siku za mwanzoni lazima utapata tabu kwa sababu unakuwa bado mgeni, hujazoeana na watu uliowakuta na wao hawajakuzoea kwa hiyo inahitaji muda kuweza kuzoeana kutengeneza marafiki wa kushirikiana nao, hii naiona kwa Alexis Sanchez pale Manchester United.”

“Ndani ya Manchester United kuna mchezaji gani ambaye anampokea Sanchez alipotoka Arsenal? Hakukuwa na mchezaji ambaye walizoeana awali. Ukiangalia kwenye kikosi cha United kuna wachezaji wawili tu ambao wanatoka Amerika ya Kusini Marcos Rojo na Antonio Valencia lakini ukiangalia kwa tabia, Sanchez ni mkorofi uwanjani mara nyingi akikutana na beki wanapogongana huwa anarudishia au anapotolewa maneno machafu huwa na kawaida ya kujibu.”

“Mara kadhaa Sanchez na Rojo walishawahi kuvurugana kwenye mechi tofauti zilizowakutanisha kwenye timu zao za taifa na Rojo ameshawahi kuthibitisha hilo, Rojo aliposikia Sanchez anakwenda United alishangaa kwa sababu ni mchezaji ambaye wamewahi ‘kuzinguana’ mara kadhaa. Sasa mtu ambaye unategemea ampe ushirikiano unakuta ndio huyohuyo haziivi kutokana na matukio yao yaliyopita.”

“Sanchez hazungumzi Kiingereza, mataifa mengi ya Amerika ya Kusini wanazungumza ki-spanish labda anaweza akawasiliana na Juan Mata na David de Gea kwa hiyo lugha gongana inaweza kuwa kikwazo kuwa karibu na wenzike lakini pia lugha haiwezi kuwa kichocheo cha kuwa karibu na wenzie ndiyo maana hata wafanyakazi wa uwanja wa mazoezi wa Unitd (Carrington) wanasema wakati mwingine wachezaji wanapokuwa mgahawani mara nyingi hukaa kwenye meza akiwa peke yake sasa inawezekana hali ya upweke inampa shida ndani ya klabu yake mpya ya Manchester United.”

“Ukiangalia kwenye kurasa za instagram utamuona sanchez yupo na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ambapo wanajiandaa na michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Denmark na Sweden, picha zinamuonesha anafuraha kwa sababu amekutana na watu ambao wamezoeana na anakuwa huru.”

“Na amezungumza kwa mara ya kwanza kwamba kuna ugumu anakutana nao kuishi kwenye klabu yake mpya kwa sababu ni mgeni na itamchukuwa muda, ilifika wakati alifikiria kuomba ruhusa kwa benchi la ufundi la timu ya taifa ili asijiunge na timu ya taifa abaki Manchester afanye mazoezi zaidi ili aweze kupunguza gap wachezaji wenzake watakapo rudi awe fit lakini akaona ni bora aende kuungana na rafiki zake waliozoeana apate fursa ya kubadilishana mawazo huenda akaondoa upweke alionao.”

Kwa sababu hizo alizozitoa Dauda ni nani anaamini sanchez atarudia makali yake kama ilivyokuwa wakati yupo kwa wazee wa mitutu Arsenal?   Au ndo yanajirudia yaliyowakuta Di Maria, Falcao, Veron Anderson baadhi ya wachezaji wa Amerika ya Kusini walioshindwa kufurukuta pale OT?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here