Home Kitaifa Kuelekea Stars vs DR Congo “Siendi uwanjani kuangalia matokeo”-Shaffih Dauda

Kuelekea Stars vs DR Congo “Siendi uwanjani kuangalia matokeo”-Shaffih Dauda

9350
0
SHARE

Kesho Jumanne Machi 27, 2018 timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mechi ya kirafiki ya kalenda ya fifa dhidi ya DR Congo ambayo ni timu ya tatu kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa viwango vya Fifa vilivyotolewa machi mwaka huu.

Tunisia inashika nafasi ya kwanza Afrika (nafasi ya 23 duniani) ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya pili (nafasi ya 27 duniani) huku DR Congo ikiwa nafasi ya tatu Afrika (nafasi ya 39 duniani).

Shaffih Dauda amesema anavutiwa na aina ya mechi za kirafiki ambazo Stars imepata kipindi hiki kwa sababu kucheza dhidi ya wapinzani walioizidi ndiyo kipimo halisi kwa timu yenye malengo ya kufika juu siku za baadaye.

“Nikiwa mtanzania, shabiki wa Taifa Stars, naiheshimu DR Congo kwamba ni timu bora, yenye uwezo na ni kipimo sahihi kwa timu yetu ambayo ina ndoto ya kupambana na kufika walipo wenzetu wa DR Congo”-Shaffih Dauda, mchambuzi wa michezo Clouds Media Group.

“Mashabiki wa Tanzania tunapenda matokeo, hakuna kitu kizuri kama kwenda uwanjani kuiunga mkono timu bila kujali matokeo baada ya dakika 90.  Hata Fifa wanasisitiza kumheshimu mpinzani, mashabiki waheshimiane, wachezaji waheshimiane na timu ziheshimiane. DR Congo ipo nafasi ya 39 kwenye viwango vya Fifa vilivyotolewa mwezi Machi 2018 lazima tuwaheshimu.”

Dauda amesemataifa stars inapocheza na timu zenye uwezo kama ilivyo kwa Algeria na DR Congo hatupaswi kuangalia matokeo pekee kama ambavyo wanafanya mashabiki wengi wa soka nchini.

“Timu inapocheza mechi kama hizi, kitu cha kwanza kabisa kuangalia ni performance ya timu ambayo pia inapimwa na matokeo. Jambo jingine mechi kama hizi huwa ni kwa ajili ya kujaribu wachezaji na kuangalia kama wanacheza kitimu na kwa kufuata mbinu na maelekezo ya kocha.”

“Unapocheza na DR Congo au Algeria unawapa uzoefu wachezaji, unawapa nafasi ya kupata ushindani wa hali ya juu ili baadaye wanapokabiliana na timu yoyote ya kiwango cha juu katika mashindano hawatakuwa na uoga kwa sababu walishakutana na mechi za aina hiyo mapema.”

“Ukiangalia pasi iliyopigwa na Mahrez katikati ya Banda na Yondani likafungwa goli la kwanza wakati stars inafungwa 4-1 na Algeria  kama hupati mechi za aina ile ni nadra kukutana na pasi za aina ile ambazo zinakuonesha makosa yenu. Ukitaka ucheze na timu ambazo hazikupi changamoto kama zile usitarajie utafanya vizuri ukikutana na timu zenye viwango vya juu.”

“Tukitaka kucheza mechi zetu ili tupate matokeo, tukikutana na timu za viwango kama Algeria tutaendelea kuchezea goli za kutosha. Mimi siendi uwanjani kwa ajili ya matokeo, naenda kuangalia mpira, ikitokea tumepata matokeo tunashangilia ikitokea tumefungwa tutulie tukubali matokeo tusianze maneno-maneno yetu ‘angekuwepo fulani’.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here