Home Kimataifa Kuelekea kombe la dunia “mashabiki 90 Uingereza wawekwa rumande”

Kuelekea kombe la dunia “mashabiki 90 Uingereza wawekwa rumande”

6658
0
SHARE

Kati ya mambo ambayo yanasubiriwa kwa hamu sana ni namna ambavyo mashabikinwa soka wa Uingereza na wale wa Urusi watakabiliana katika michuano ya kombe la dunia inayotarajia kuanza hivi karibuni nchini Urusi.

Kumekuwa na ugomvi wa muda mrefu kati ya pande hizi mbili na jambo kubwa linaloonekana hapa ni ubabe wa mashabiki wa Uingereza ambao mara nyingi wamekuwa wakionekana vinara wa ugomvi.

Jana kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Uingereza na Uholanzi waliokuwa nyumbani, kama kawaida Waingereza wanaonekana ni wale wale kwani wamefanya kile kinachotarajiwa watakifanya Urusi.

Walileta fujo na hii ilikuwa kabla ya mchezo wao dhidi ya Uholanzi, polisi jijini Amsterdam wanasema mashabiki 90 walikamatwa wakati wa fujo hizo na wote wamezuiwa kurudi nchini kwao wakisubiri hatua kubwa zaidi kuchukuliwa.

Kwanza walikamatwa mashabiki 70 kutoka Uingereza lakini baadae kuliongezeka kundi lingine ambao wengi walionekana mtaani wakiwa wamelewa na kufanya fujo kila walipopita kuelekea uwanjani.

Mashabiki hao hawakuanza fujo jana kwani siku ya Alhamisi pia kuna kundi la mashabiki wa taifa hilo wanadaiwa kuingia nchini Uholanzi na kuanza kuleta fujo usiku wa kuamkia siku ya mchezo wenyewe.

Shukrani kwa nyota wa Machester United Jesse Lingard ambaye alifunga bao pekee katika mchezo huo wa kirafiki ambao uliisha kwa wageni kuibuka kidedea kwa bao 1 kwa nunge.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here