Home Makala Zlatan ashushwa daraja, amkana Rafiki yake kisa umaarufu

Zlatan ashushwa daraja, amkana Rafiki yake kisa umaarufu

7091
0
SHARE

Sehemu ya tatu; Simulizi inayolezea maisha ya Zlatan Ibrahimovic


Na Priva Abiud

Ilipoishia….

Mungu sio athumani wakiwa nyuma magoli 2-1, dakika ya 93 Malmo FF walizawadiwa mkwaju wa penati. Uwanja mzima ulilipuka. Zlatan akiwa na magoli 12 tayari mashabiki waliamini mfungaji wao bora atakwenda kuwatoa kwenye mdomo wa mamba. Palitokea sintofaham kwa sababu mwalimu alikuwa amekwisha kumpanga Tony Flygare kama mpiga matuta. Mashabiki walipiga makelele wakimtaka Zlatan akapige tuta.


Mwalimu alifanya maamuzi kuwa Tony ndiye anayepaswa kupiga tuta lile. Nilitazama jukwaa la kushoto lilopo upande wa kusini lijulikanalo kama Panorama mashabiki walikuwa mavua mashati wengine walikuwa kama wamechanganyikiwa. Kilichoniumiza ni kwamba wengi walitaja jina langu wakihitaji mimi kwenda kupiga penati hiyo.

Zlatan alitamani kufumba macho asione kile kitakachotokea. Ni kweli, mkwaju ule ulidakwa, na ndipo safari ya Zlatan kwenda ligi daraja la pili ilishika kasi. Tony alisimama kama amegandishwa.
Zlatan anasema alimlaumu sana rafiki yake Tony flygare kwa kuishusha Malmo FF daraja. Aliona ni kama jua limeshuka kilometa kadhaa kwa namna alivyohisi joto. Tony alikuwa na umri wa miaka 17 tu na alikuwa na kipaji kikubwa sana lakini kwanini akose penati? Nilijiuliza sana. Ilikuwa ni penati ambayo ingeiokoa Malmo FF kushuka daraja. Uwanja mzima ulizizima huzuni kuu. Zlatan aliamua kumfuata Tony hakumuonea haya alimtukana sana Tony bila uoga wowote.

Tokea pale maisha ya Tony kwenye soka yalipotea. Zlatan alikiri kuwa Tony alikuwa na kiwango bora kumzidi. Lakini mkwajua wa penati uliharibu taswira nzima ya maisha yake kisoka. Rafiki yake Zlatan hakuwahi kupata tena nafasi katika vilabu vikubwa. Kitendo kile kilimuuma sana Zlatan.

Tony alikwenda kucheza vilabu kama Assyriska ya huko huko nchini Sweden, Wehen Wiesbaden ya nchini ujerumani na FK Cementarnica iliyopo nchini Macedonia.
Tony akiwa anacheza Ujeruman alimtumia Zlatan Meseji. Zlatan akamuuliza wewe ni nani, Tony Akamjibu “mimi Tony rafiki yako wa Malmo FF”, Zlatan “Tony yupi? Sikukukumbuki wala sikufahamu”. Tony akamjibu “huwezi kuwa siriazi, hunifahamu mimi? Tumecheza wote Malmo? Acha utani ndugu yangu”. Zlatan Kimya (hakujibu)

Akajaribu kumkubushia maisha yao ya nyuma, “ulinitukana kwenye vyumba baada ya kukosa penati mechi ya Mwisho? Zlatan (kimya). Zikapita siku mbili. Tony akaamua amtolee povu akamuandikia ujumbe mzito, akamwambia kuwa

najua una maisha mazuri, naheshimu sana nafasi yako kwa taifa letu, natambua umaarufu wako na ufanisi wako kwa sasa, mimi sikuombi hela, nakuheshimu, na najivunia kukujua na kuwa mtu ambaye tunafahamiana, na kama ikitokea tukionana siku moja nitakutana tusi lile lile uliloniita baada ya mimi kukosa penati (sitokuogopa), ila usinidharau mimi hivyo hata kama sina maaisha au umaarufu kama wa kwako, niheshimu tu kama tulivyoheshimiana hapo awali”

Tony alifahamu fika Zlatan ana kiburi na jeuri. Ni mtu waliyekuwa nae utotoni. Tony ni mtu pekee aliyemtetea Zlatan kila alipokosea. Ilibidi wasaa mwingine alimsaidia adhabu na Zlatan kila mara ilipotokea amekosea.

Tony kesho yake asubuhi aliamka mapema na kutazama simu yake akiamini kuwa atakutana na majibu. Lakini hola. Muda ule ilikuwa imepita miaka 13 Tony Zlatan kuonana. Mara ya mwisho kuonana na Zlatan ilikuwa jijini Stockholm kwenye supamaketi. Wakati huo Zlatan alikuwa na timu ya taifa.

Tony hakukata tama kumtafuta rafiki yake huyu wa utoto ambaye kwa sasa mashabiki zaidi ya million 600 duniani wanamfahamu.

Akamtumia meseji kwa mara nyingine akiamini itajibiwa kwa sababu alikuwa hapokei simu. Akamwambia “kumbuka zamani mimi nilikulipia tiketi yakuingia uwanjani kule Zigge na baba yangu alitubeba na gari yake mpaka Trellebrorgs wakati wa mchezo dhidi ya Blackburn mwaka 1994”.

Hakika Zlatan na Tony walikuwa kama Pwagu na Pwaguzi.

Waliishi pamoja tokea wakiwa na miaka 6. Zlatan aliwahi kuharibu basikeli ya baba yake Tony na alimdhulumu Tony baiskeli nyingine mbili. Maisha ya umaarufu yalimtenga kabisa na rafiki yake. Amini usiamini urafiki una nguvu kuliko umaarufu, baada ya siku kadhaa Zlatan alimtumia meseji Tony na kumwambia “nipeleke mahali ambapo wafalme wanakula”. Na hiyo ilikuwa mara ya pili kwa wao kuonana. Baada ya kuonana walipigana

imeandaliwa na Priva ABIUD 0763370020

chini ni link zinazonesha makala zilizopita kama hukuzisoma.

Sehemu ya Kwanza

Zlatan aamua kuachana na soka atafutwa kwa wizi

sehemu ya pili

Zlatan Apigana Uwanjani, adai anampenda baba kuliko Mama

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here