Home Ligi EPL Habari mbali mbali majuu

Habari mbali mbali majuu

6653
0
SHARE

*Morrison Aitosa England,Akimbilia Jamaica*

GUADALAJARA,Mexico

*MCHEZAJI* wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, amethibitisha kwamba yupo tayari kujiunga na Timu ya Taifa ya Jamaica.

Morrison mwenye umri wa miaka 25, ambaye sasa anachezea katika klabu ya Atlas kwa mkopo akitokea Lazio, aliyasema hayo Jumanne na akisisitiza kwamba chaguo pekee kwake ni kujiunga na Jamaica katika ngazi ya kimataifa.

Tayari Morrison aliweza kuichezea England katika ngazi ya vijana chini ya umri wa miaka 21, na sasa yuko mbioni kukamilisha suala hilo na Shirikisho la Soka la Jamaica katika siku zijazo.

*Chiellini Aondoshwa Katika Kikosi Cha Italia*

TURIN,Italia

*JUVENTUS* imetoa taarifa rasmi juu ya jeraha ambalo amelipata Giorgio Chiellini,katika mchezo uliochezwa Jumamosi dhidi ya Spal.

Wamesema kwamba mchezaji huyu ataendelea kuwa mapumzikoni, baada ya kuumia misuli ya paja katika mguu wake wa kulia.

Hivyo Timu ya Taifa ya Italia imeamua kumuondoa katika kikosi ambacho kinatarajia kucheza na Argentina pamoja na England, lakini huenda pia ikaleta sura nzuri kwa Juventus maana Machi 31 watakuwa na mchezo dhidi ya Ac Milan na mchezaji huyo atakuwa amerejea kikosini tayari.

WORLD CUP 2018*

*Bertrand Atupwa Nje Katika Kikosi Cha England*

SOUTHAMPTON,England

*BEKI* wa kushoto Ryan Bertrand ameondolewa nje ya kikosi cha England,kutokana na suala lake la nyuma la kiafya.

Mchezaji huyo anayecheza katika klabu ya Southampton, alitajwa katika kikosi cha wachezaji 27 kwaajili ya michezo miwili ya kirafiki katika maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia.

Taarifa kutoka Chama cha Soka England inasema “Mchezaji huyo amerudishwa katika klabu yake kwaajili ya tathimini ya jeraha lake alilolipata nyuma”.

Hivyo Bertrand atalazimika kukosa mchezo wa Uholanzi na Italia,Lakini bado haijawa tatizo kwa kikosi cha Southgate maana Ashley Young na Danny Rose watasimama katika nafasi hiyo ya kushoto.

Zimeandaliwa na: *Daniel S.Fute (Official DSK)*

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here