Home Kimataifa Baada ya Wilfred Zaha, Ivory Coast wapata pigo jipya ni Yaya Toure

Baada ya Wilfred Zaha, Ivory Coast wapata pigo jipya ni Yaya Toure

7023
0
SHARE

Nyota wa Crystal Palace Wilfred Zaha hataweza kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Ivory Coast kwa kile kinachotajwa kuwa ni majeruhi, lakini sasa timu hiyo ya taifa ya Ivory Coast imepata pigo jipya.

Ni Yaya Toure, kiungo huyo wa Manchester City hatakuwa na timu yake ya taifa ambayo aliitosa miaka mitatu iliyopita na baadae kurejea tena lakini safari hii matatizo ya kifamilia yanamuweka tena mbali na timu.

Ivory Coast wanajiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Togo na Molodova michezo ambayo inatarajiwa kupigwa nchini Ufaransa mwezi huu tarehe 24 na 27 lakini Yaya sasa hataweza kuitumikia timu hiyo katika michezo hiyo.

Toure ameichezea Ivory Coast michezo 102 hadi sasa na alikuwepo katika kikosi cha Ivory Coast kilichobeba kombe la CAF mwaka 2015, lakini mwaka huu timu yake haitakuwepo kombe la dunia ikiwa ni mara ya kwanza kutokuwepo tangu 2002.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here