Home Uncategorized Road 2 World Cup: Sababu 6 kwanini Switzerland watafuzu kucheza robo fainali

Road 2 World Cup: Sababu 6 kwanini Switzerland watafuzu kucheza robo fainali

5143
0
SHARE
Watanzania tupo million 50 lakini kombe la mataifa ya afrika ni kizungumkuti, cecafa yenyewe tia maji tia maji. Uswisi idadi kubwa kabisa ya watu haizidi million 8. Yaani ni mikoa miwili tu ya Tanzania. Uswisi wapo kombe la dunia. Uswisi imewahi kufika robo fainali mara tatu katika michuano ya kombe la dunia. Sisi ikiwa ndoto yetu kubwa ni cecafa na kombe la mataifa ya afrika ambayo bado siwezi hata kuiita ndoto.

Wasifu wa Uswisi

Jina la Utani; Schweizer Nati (Swiss Nati), La Nati (The Nati),

Rossocrociati (literally Red Crusaders)

Kocha mkuu; Vladimir Petkovic

Nahodha; Stefen Lichtsteiner

Mfungaji bora; Alexander Frei (42)

Shirikisho : Swiss Football Federation

Nafasi Viwango vya FIFA (13)

Fifa imetoa takwimu kuonesha ni kivipi mwaka huu Uswisi inaweza kuvuka hadi hatua ya robo fainali ya kombe hili.

Rekodi nzuri katika hatua ya kufuzu.

Walifuzu kwa njia ya mtoano baada ya kuifunga Ireland ya kaskazini goli moja ugenini baaa ya kutoka suluhu nyumbani. Waliweza kumfunga bingwa wa ulaya Ureno magoli mawili kwa bila waliweza kushnda michezo 8 iliyofuata kabla ya kupoteza mchezo wa mwisho uliopelekea wao kucheza hatua ya mtoano.

rodriguez

Upinzani thabiti dhidi ya timu kubwa

Switzerland watakutana na mabingwa wa kihistoria wa kombe la dunia brazil mnamo tarehe 17 June mjini Rostov. Wadukuzi wa mambo wanadai huu ani mtihani mgumu sana kwa kocha Vladimir Petkovic. Ingawa isiwe kazi sana kwao kwani mwaka 2006 uswisi waliwazamisha suluhu mabingwa wa kombe la dunia mwaka 1998 Ufaransa katika mji wa Stuttgart, usishangae sana kwani mwaka 2010 kule kwa madiba walisimamisha makelele ya wahispaniola kwa kuwazaba goli moja kwa mtungi.

Na katika hatua hii ya kufuzu kombe la dunia walimbabua Cristiano Ronaldo na Ureno yake fimbo mbili bila majibu. Hata mwaka 2016 kwenye michuano ya kombe la Yuro walimlazimisha mfaransa kwa suluhu tasa katika kiwanja cha Stade Pierre-Mauroy, Villeneuve-d’Ascq mbele ya mashabiki 45,616. Katika hatua ya mtoano walitoka sare ya mabao moja kwa moja kabla ya kuslubishwa kwa mikwaju ya penati dhidi ya Poland.

Mfumo wao wa uchezaji

Kwa kipindi cha miaka 20 Uswisi imekuwa ikicheza zaidi kitimu na kuzipa ugumu sana timu ngumu barani ulaya. Wanacheza kama siafu au mchwa. Wamekuwa wakijituma. Hawaangalii sana mpinzani anayecheza nae yupoje ila wanachokiangalia ni kwa vipi wao wapate matokepo tu. Kocha wao mkuu Petkovic anasema kuwa wao wanategemea sana mpinzani wake yupo na hali gani. Wanaweza kuanza mchezo kwa kasi ndogo lakini pia wanaweza kubailika katikatik ya mchezo. Kiujumla hii ni timu ambayo ni ngumu sana kuitabiri.

PATA KIFURUSHI

Albania ina wacheazji 6 ambao ni wazaliwa wa Uswisi; Arlind Ajeti, Freddie Veseli, Migjen Basha, Amir Abrashi, Shkelzen Gashi na Taulant Xhaka

Uswisi ina wachezaji 6 ambao ni wazaliwa wa Albania; Xherdan Shaqiri, Granit Xhaka, Admir Mehmedi, Shani Tarashaj, Blerim Dzemaili na Valon Behrami

Matarijio makubwa ni chachu ya kujiamini

Wamekuwa na mataraji makubwa kuliko uwezo wao. Aina hii ya imani imejengeka miongoni mwa wachezaji kitu ambacho kimepelekea timu hiyo kuwa na mafanikio yaliyozidi hata uwezo wao. Kujituma kumwefanya timu nzima iweze kumuu kila aina ya resha wanayokumbana nayo. Wamekuwa na wachezaji wenye uchu mno kama Granit Xhaka. Xhaka anasema furaha kubwa aliyo nayo ni kwamba kikosi chao chote kinajumuisha mastaa wa vilabu mbalimbali barani ulaya

Mlinda mlango imara

Nadhani unamfahamu Vyema Oliver Khan, najua pia huwezi kumsahau Jens lehman, achilia mbali Ter Stegen pia nina imani unamfahamu Manuel Neuer. Ujerumani inahesabika moja ya mataifa ya yanayozalisha walinda lango bora duniani. Tukiachana na Ujerumani, uswisi ni taifa linaloaminika kuwa lina alinda lango bora pia. Yupo Yann Sommer (Borussia Monchengladbach), Roman Burki (Borussia Dortmund) na Marwin Hitz (Augsburg) magolikipa wpte hawa ni machaguo namba moja katika vilabu vyao. Ni mataifa machache yenye uwezo wa kuwa na magolikipa watatu ambao wote ni walinda lango namba kwenye vilabu vikubwa.

imeandaliwa na Priva ABIUD  0763370020

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here