Home Kimataifa Msuva baada ya kufuzu hatua ya makundi klabu bingwa Afrika

Msuva baada ya kufuzu hatua ya makundi klabu bingwa Afrika

7172
0
SHARE

Michezo ya vilabu bingwa Afrika raundi ya pili michezo ya marudiano ilishuhudia mtanzania Simon Msuva akifanikiwa kufuzu kucheza hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yake akiwa na klabu ya Difaa Hassan el Jadida.

Mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano ya klabu bingwa Afrika Msuva alifanikiwa kufunga goli pekee na la ushindi kwa timu yake dhidi ya As Vita Club ya DR Congo timu yake ilipocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, katika mchezo wa marudiano timu yake ikalazimisha sare ya kufungana 2-2 ugenini.

“Nimefurahi kuingia kwenye hatua ya makundi kwa sababu kila timu ilikuwa inahitaji kufika kwenye hatua hiyo lakini timu nyingine zimeshindwa na pia tunajipanga kushindana kwenye hatua hiyo kwa sababu ni hatua nyingine tutakayokutana na timu ambazo zimepambana hadi kufika hatua hiyo hata huko tutashindana”.

Msuva amesha cheza hatua ya makundi ya michuano ya Afrika lakini ilikuwa ni Confederation Cup akiwa  na klabu yake ya zamani ya Yanga lakini sasa atacheza kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here