Home Kimataifa Road 2 World Cup: Baada ya miaka 16 – Senegal wanarejea World...

Road 2 World Cup: Baada ya miaka 16 – Senegal wanarejea World Cup – nini matarajio yao?

5312
0
SHARE

Aliou Cisse aliichezea Senegal michezo 35. Kiungo huyu aling’ara sana michuano ya mwaka 2002 FIFA kule nchini Korea/Japan na ameitumikia senegal kama mkufunzi tokea mwaka 2015

Bila shaka Senegal mwaka 2002 walikonga nyoyo za walio wengi. Timu yao ya taifa inajulikana kama Les Lions de la Teranga yaani Simba wa Teranga. Walileta hamasa kubwa kwa mashabiki wao hasa kwa aina ya uchezaji wao wa kuvutia sana.

Nahodha Aliou Cisse alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemezi kabisa kwenye meli yao hiyo iliyotua Nanga hatua ya Robo fainali. Alikuwa mpiganaji, mpambanaji na shujaa. Kivutio kikubwa ilikuwa aina yake ya unyoaji iliyojulikana kama (reggae style)

Ni miaka 16 imepita sasa Cisse anaungana tena na wana Senegal wenzake kwenye michuano hii mikubwa kabisa duniani inayotazamwa na watu zaidi ya bilioni 1. Kwa sasa hatokuwa tena uwanjani ila yupo benchi anacheza kwa maneno na mipango.

Wasifu

Majina Kamili Aliou Cissé
Tarehe ya Kuzaliwa 24 March 1976 (age 41)
Sehemu alipozaliwa Ziguinchor, Senegal
Kimo 1.80 m (5 ft 11 in)
Nafasi Uwanjani Midfielder/Defender
Kazi: Kocha mkuu wa Senegal

Kocha huyu ametanabaisha mambo makuu Manne.

Vizazi Viwili tofauti Je Malengo yapo sawia?

“ni miaka 16 imepita sasa tokea 2002, hatukuwahi kushiriki tena kombe la dunia. Mataraji ya wengi walidhani tulipaswa kuwa washiriki wa kombe la dunia mara mara, hilo sio suala nyeti sana kwetu. Hatimaye tumerudi tena, ni jambo jema. Tulijiandaa muda mrefu na tumefanikiwa kurudi.“tunatarajia kufikia tena hatua ya Robo Fainali tusipofika pia sawa. Tuna wachezaji wachanga na wenye uwezo mkubwa. Wenye shauku ya mafanikio, tatizo ni uzoefu wa michuano mikubwa. Tutapambana mpaka dakika ya mwisho, sisi ni waafrika, tutacheza kama waafrika, tutalinda soka letu, hatutaiga mfumo wa mataifa mengine” Cisse

Wachezaji Chipukizi na ufanisi wa Vipaji vyao?

“ wachezaji wa changa sio tatizo. Unakumbuka 2002, tulijikuta kwenye kundi moja na Ufaransa, mabingwa hawa wa soka la ulaya, na mabingwa wa soka duniani, tukakutana na Uruguay na Denmark. Ila haikuzuia sisi kufika mbali. Uchanga sio tija. Cha msingi kujituma na kujitambua. Hatukumdharau na hatukumuogopa mtu. Kila mtu alicheza mpira wake. Kikubwa ilikuwa kutazama zaidi malengo yetu na sio fulani anacheza vipi. Sisi hilo halituhusu. Nachohitaji kwa vijana wangu ni kucheza katika mtizamo huo huo. Tucheze sisi kama sisi. Achana na hayo hayatuhusu sisi.

Vipi kuhusu washindani wake, Poland, Japan na Colombia?

Kundi letu sio gumu, ubora wa timy zetu unalingaa sana ingawa kuna kaugumu kwa kiasi fulani. Colombia wasitutishe sana kisa eti walifika robo fainali 2014 kule Brazil! Poland ni moja ya timu 7 bora dunia, sio wa kuwabeza. Halafu hapo sasa ndio unakuja Senegal na Japan. Ukweli kila mtu atajitahidi kwa uwezo wake, sisi tunakwenda kutibua mipango basi. Hatutaki kujifananisha sana na wengine maana lengo letu sio hilo. Tuone itakuwaje.

Upi Ufanisi wako ? Kama kocha au mchezaji?

“Mhhhh nadhani kama kocha (kisha akacheka) nadhani ni kama kocha. Najivunia kuwa sehemu kubwa ya historia ya taifa hii na nia ndoto zaidi ya kufanya hivyo kama kocha. Muda ndio huu. Nahitaji kujenga historia kubwa zaidi. Hakuna namna. Sisi ni bora. Na tutadhihirisha hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here