Home Makala Unafiki wa Camp Nou utamezwa na Kombe la dunia

Unafiki wa Camp Nou utamezwa na Kombe la dunia

12072
0
SHARE

Tiketi ya Urusi

Mesut Ozil aliondoka Real Madrid, kila mtu alisikitika kwa maamuzi yale. Sababu za kuuzwa kwake zilikuwa na figisu Figisu. Naweza kusema yalikuwa mamuzi ya Florentino Perez. Hakujali ufundi wa Ozil ila kuna kitu alikihitaji zaidi. Alihitaji kilichofanyika Stamford Bridge kwa Steven Gerrard kifanyike kwake. Aliumia sana mwaka 2005 pale Ronaldinho alipoibuka shujaa Bernabeu (watu wa Madrid sio wanafiki, walimpigia Dinho makofi). walishindwa kuvumilia alichofanya Ronaldinho, chuki ziliwajaa lakini mikono yao iliwawasha. Kiroho safi.

Wachezaji watano wamekwisha kuondoka na heshima Bernabeu, mwaka 2005 Ronaldinho, hata hasimu wao mkubwa Lionel Messi mwaka 2009 nae aliibuka Mfalme Bernabeu ilibidi tu wampigie makofi. Del Piero pia hakuwaacha salama. Mwaka 2015 unafiki uligeuka ukawa unga, lakin maji yalizidiwa, Ilibidi wamwage mboga wapike uji. Walipata kichapo, na bado walisimama na kumpigia Iniesta Makofi.

Hayupo, na simjui aliyewahi kupigiwa makofi Camp Nou kutoka Madrid.

Stefano Relando aliandika kwa herufi kubwa kwenye gazeti la mjini Madrid, akasema “Isco ni lulu ya baadae kwa Wahispania”. Huenda Perez aliposoma hiki kichwa cha habari alitabasamu na alijiamini sana. Hakujali kuwa kuondoka kwa Ozil kutaleta pengo.

Kwa bahati mbaya Matarajio ya Perez kwa Isco yalianza kukauka. Isco alikuwa na misimu mibovu. Alianza vibaya mno. Kila mtu alianza kumtukana. Ujio wa Zinedine Zidane ulibadilisha maisha ya Isco. Alimpa uhuru ambao wengi hawakutarajia. Mabadiliko makubwa kwenye ufanisi wa Isco yalionekana.

Takwimu zinasema Kwa miaka kadhaa Madrid imecheza bila kuwa na kiungo wa kihispania aliyekuwa na uhakika wa namba klabuni hapo baada ya kuondoka akina Guti na Xabi Alonso.

Huenda Isco ameziba pengo. Kubali ukate urithi wa Andreas Iniesta kwenye timu ya taifa kwa sasa upo kwenye umbo la Isco. Isco ni mchoyo, sawa…, anaupenda mpira kuliko anavyowapenda wachezaji wenzake, sawa.., lakini ni mgumu sana kumnyang’anya mpira mguuni mwake. Ana mguu kama kijiko, anautumia kupakua na kulia. Alichonyimwa ni jicho la tatu ambalo Iniesta analimiliki (kutoa pasi muhimu na kwa wakati). Kwa misimu miwili Zinedine amefanikiwa kumrudisha Nondo aliyetekwa na umaarufu.

Madrid ilikosa kiungo msumbufu kutoka Hispania. Ilikosa mtu mwenye soka la jadi ya kispanyola. Walitawaliwa sana. Kwenye michezo ya hivi karibuni ya Barcelona na Madrid isco na Assensoo walitawala sana, ila waliishia kuzomewa tu. Huenda wasimpigie Assensio, sawa, huenda wasimpigie Vasquez sawa, huenda pia wasimpigie makofi Isco kwa kuwa alisema barca ni wabaguzi.

Lakini kubali ukatae kama Mashabiki wa Liverpool walishindwa kumpigia Cristiano Ronaldo Makofi akiwa na Man utd ila roho ziliwasuta wakampigia makofi akiwa na Real Madrid pale pale Anfield. Hivyo huenda mashabiki wa barca wakampigia Isco makofi akiwa na timu ya taifa. Kombe la Dunia hilo hapo. Ni wakati wa Isco kuonesha yeye ni mhispanyola.

Huenda Furaha aliyo nayo Perez kuona kiwango cha Isco kinavyokua hata leo tukimfuata tukimwambia atulipie deni la bombadier anatulipia na anatuongezea nyingine. Isco alitukanwa sana mwacheni Perez acheke, msipompigia makofi tabasamu la Perez linamtosha Isco na Kombe la Dunia anajua wanafiki watakuwa wamevaa jezi yake.
Imeandikwa na Priva ABIUD 0763370020

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here