Home Kitaifa Mzee wa ‘always next time’ ameanza kwa ushindi

Mzee wa ‘always next time’ ameanza kwa ushindi

7154
0
SHARE

Leo Machi 18, 2018 kocha mkuu wa wa muda wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngoro ngoro Heroes’ Ammy Ninje ameiongoza timu hiyo kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya vijana wenzao wa Morocco katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa dakika ya 62 na Muhsini Makame kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Morocco kuushika mpira kwenye penati box.

Ngorongoro Heroes itacheza tena mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Msumbiji siku ya Jumatano Machi 21, 2018.

Mechi hizo za kirafiki ni maandalizi ya Ngorongoro Heroes kuelekea mchezo dhidi ya DR Congo kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (AFCON U20).

Mchezo dhidi ya DR Congo utachezwa Machi 31, 2018 kwenye uwanja wa taifa kisha itasafiri kuelekea DR Congo kucheza mechi ya marudiano inayotarajiwa kuchezwa wiki mbili baada ya mechi ya awali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here