Home Makala Gerrard na Lampard hawana meno

Gerrard na Lampard hawana meno

11675
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Ni miaka Takribani 25 imepita tokea ligi kuu England iundwe upya mnamo mwaka 1992. Lakini miaka 7 nyuma, kunako mwaka 1985 pale Liverpool palitokea Maafa. Uwanja wa Heysel ulianguka na Kocha Joe Fagan aliamua kujiuzulu.

Fagan alipoamua kujiuzulu mwaka ule ule, Kenny Dalglish legend wa kukumbukwa milele pale Liverpool alichukua mikoba yake akiwa kama kocha mchezaji. Alipata mafanikio mengi tu akiwa kama kocha na mchezaji ndani ya liverpool.

Ligi kuu England kuna kitu nmekiona. Ukiitazama ligi kuu Hispania, inazalisha matunda mengi mno.

Wakati England ikitoa Wachambuzi wazuri wa soka, kama akina Gary Leeniker, Garry Neville, Owen, Henry, Scholes kule Hispania wao wanazalisha makocha wenye mafanikio makubwa mno. Hispania pia wachambuzi wapo kama Kocha na mchezaji wa zaman wa Klabu ya Real zaragoza Babu Jorge Valdano anayefanya kazi Bein Sport.

Tokea mwaka 1992 England ni Makocha 9 tu walioshinda kombe la ligi kuu ( Alex Ferguson, Carlo Ancellot, Kenny Daliglish, Arsene Wenger, Manuel Pellegrin, Roberto Mancinni, Cladudio Ranieri, Jose Mourinho na Antonio Conte) huenda pia na Bingwa Mteule Pep Guardiola.

Kati ya hao wote waliocheza ligi kuu England ni Keny Daliglish tu. Mancinni hatuwezi kumweka kwenye kundi hili kama zao la ligi kuu England kwa sababu, alikuja Leicester City akiwa na miaka 36, hakucheza hata mechi moja dakika 90, pili alicheza michezo mitano tu kisha akaenda Kuwa kocha Fiorentina. Hivyo alikuwa kama mpita njia.

Hivyo takwimu hizi tukimweka Mancinni pembeni hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kucheza England zaidi ya Dalglish aliyetwaa kombe hilo akiwa kama kocha wa Blackburn rovers mwaka 1993.

Upande wa La liga, tokea mwaka 1992 ( Johan Cruyjff alicheza Barcelona na alitwaa la liga mwaka 1992,

Jorge Valdano aliyeicheza Real Zaragoza na Real Madrid alitwaa laliga 1994, Radomir Antic, pia yupo babu Del Bosque mzaliwa wa Salamanca aliyepata mafanikio makubwa sana miaka ya 2000 akiwa na Real Madrid.

Rafael Benitez hakucheza sana Daraja la juu ingawa alicheza ndani ya Hispania katika klabu za Real Madrid C, Castila n.k nae alitwaa ubingwa wa La liga akiwa na Valencia. Frank Rijkaard nae aliwahi kuichezea Real Zaragoza na kutwaa la liga akiwa na Barca (huyu nae sio zao muhimu la la laliga kwani licheza kwa mkopo Zaragoza kwa mwaka mmoja.

Sina haja ya kuwazungumzia Pep Guardiola, Zidane Zinedine, Luis Enrique na Diego Simeonni pamoja na Marehemu Tito Villanova hawa wanafahamika kuwa wote wamechezea vilabu walivyobebea nazo makombe, pamoja na Babu Ben Schuter.

Makocha 12 waliowahi kucheza laliga tayari wametwaa la liga. Kwa Upande wa England ni Keny Dalglish tu ndiye mwenye medali akiwa kama mchezaji na pia kama kocha ndani ya ligi kuu England.

Makocha wengi wamejaribu kama akina Mark Hughes, Sam Allardyce na wengine wengi wameshindwa. Wachezaji wengi waliocheza England kwa muda mrefu wamekuwa wapondaji tu kwenye vituo vya Tv. Garry Neville alijaribu lakini yaliyomkuta hayana tofauti na yale yaliyomkuta baba yetu mzee Kitwanga.

Tazama akina Gerrad na Rio, wamejificha nyuma ya kioo cha BT sports Tv, ili kuponda wenzao kila kukicha. Lampard juzi nae kakimbilia huko huko. Sijajua hasa kwanini hawafuati nyayo za akina Zidane, Guardiola na Enrique.

Hivi ndivyo utamaduni wa la liga unatunzwa na kukua. Hii ndio sababu kubwa ya vilabu ya La Liga kutokuporomoka sana kwa sababu vizazi vile vile vinatunza tamaduni za vilabu husika.

Imeandikwa na Priva abiud
0763370020

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here