Home Uncategorized Tuwasikie makocha wanasema nini kuhusu robo fainali Champions League

Tuwasikie makocha wanasema nini kuhusu robo fainali Champions League

7957
0
SHARE

Tayari droo ya robo fainali ya michuano ya Champions League imeshatoka, miamba 8 itachuana kutafuta wababe wanne wa kucheza nusu fainali, lakini makocha wanasemaje kuhusu droo hiyo?

Jurgen Klopp

“Nilijua tu tunaweza kupangiwa Man City. Na hii ilikuwa droo ya ndoto za mashabiki wengi wa Man United. Tunajiandaa vyema kabla ya kukutana na Man city. Najua hatupewi nafasi kubwa kusonga mbele lakini kwenye harua ya Robo fainali ni timu chache zenye uhakika wa kusonga mbele. Baada ya mimi kupangiwa na Man City niliangalia uso wa mkurugenzi wa Man City inaonekana wazi hakupendezwa kabisa na droo hiyo, ni wazi nae ametambua ugumu wa mchezo huu”

Eusebii Di Francesco
Baada ya Francesco Totti kutoa mtazamo wake kwenye droo ya Barcelona dhidi ya Roma kocha mkuu wa Roma nao amesema kwamba “hatua hii ya mtoano imetukamata pabaya, tumepangwa na upande ambao ni mgumu zaidi duniani tena wakiwa na mchezaji hatari mno (Lionel Messi) kimsingi tutajituma, na wachezaji wangu wanapaswa kujitambua na kuhakikisha kuwa wanajitolea kwa hali na mali kuona tutapata nini.  Kujiamini ndio kitu pekee kitakachotufanya tusonge mbele”

Jupp Hyckness

Thomas Muller amesikika akisema kuwa “Sevilla hawakutwaa Kombe la Europa kwa bahati mbaya mara tatu. Walistahili. Lakini sisi ni Bayern hilo sio tatizo kwetu. Lakini kocha wa Bayern nae hakukaa kimya amesefia kiwango cha Seville. “Sevilla ni timu nzuri, wana wachezaji wenye uwezo na wenye vipaji, tunachofanya sisi ni kutazamia mchezo huu na kujua tutafanyaje. Mashabiki wao wanaipenda klabu yao na hawatakuwa tayari kuona timu yao inazidiwa hivyo watawapa moyo. Hii itakuwa ni Instabul kwa Sevilla” hata hivyo Ribery amesema hajawahi kucheza na Sevilla hivyo hii ni mara yake ya kwanza. James Rodriguez nae amesema Buyern Munich ndio timu pekee inayoweza kutwaa ubingwa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here