Home Kimataifa Sanchez anaangamia, shida ni Mourinho au amechoka?

Sanchez anaangamia, shida ni Mourinho au amechoka?

7822
0
SHARE

Ni jambo la kusikitisha sana na ambalo halikutarajiwa na wengi pale Manchester United walipoondolewa katika michuano ya Champions League haswa na timu ambayo haikupewa nafasi kubwa kama Sevilla.

Kumekuwa na matatizo mengi yanayoikabili United siku za usoni, kwanza kulikuwa na tatizo kubwa la ulinzi(lipo hadi leo) lakini pia yapo matatizo ya mchezaji mmoja mmoja kama ilivyokuwa Paul Pogba.

Na sasa Alexis Sanchez, mshambuliaji huyu wa Chile kwa sasa sio Sanchez yule ambaye tulikuwa tukimuona alipokuwa Arsenal. Sanchez huyu amekuwa hashambulii sana na hata umiliki wake wa mpira umepotea.

Katika mchezo dhidi ya Sevilla ambao United walihitaji matokeo, mbinu za Jose Mourinho zilionekana tofauti sana kwani mda mwingi Sanchez alionekana akicheza nyuma sana kutoka lango la wapinzani.

Sanchez anaonekana kutoisaidia sana timu haswa isogeapo mbele lakini pia umiliki wake wa mpira umepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na alipokuwa Arsenal na hili linaonekana kuwa tatizo siku hadi siku.

Mchezo vs Sevilla Alexis Sanchez alipoteza umiliki wa mpira mara 20, hii ilikuwa idadi yake kubwa kabisa katika Champions League kukosa umiliki japokuwa katika EPL amekuwa akipoteza mipira zaidi.

Mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Newcastle Sanchez alipoteza mpira mara 36 na alikuwa mchezaji wa United aliyepoteza mpura mara nyingi zaidi katika mchezo huo na bado amepoteza zaidi.

United vs Crystal Palace Sanchez alipoteza mpira mara 33 lakini hajaishia hapo, katika mchezo wa FA dhidi ya klabu ya daraja la chini la EPL ya Yeovil Sanchez alipoteza mpira mara 31 katika mchezo huo.

Kwa ujumla tangu Alexis Sanchez ajiunge na Manchester United amepoteza jumla ya mipira 582 na hii inamfanya Sanchez kuwa katika nafasi ya tatu ya wachezaji ambao wamepoteza sana mipira EPL.

Ufungaji wa Sanchez pia umekwama, akiwa Arsenal alikuwa akifunga kwa wastani wa 0.42 lakini United sasa amekuwa na wastani wa 0.17 kwa dakika 90, mashuti akiwa Gunners ni 4.12 lakini United ni 2.12 kwa dakika 90.

Chance alizotengeneza na Arsenal ni 3.05 huku United ni 1.53 kwa dakika 90, yote haya yanamfanya nyota huyu kuonekana kama hastahili kulipwa kile ambacho analipwa United kwa sasa (£600,000).

Mourinho anaonekana tatizo kwa Sanchez kwani tofauti na Wenger ambaye alimpa uhuru Sanchez kufanya chochote uwanjani, kwa sasa Sanchez anaonekana hadi kukaba akiwa na Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here