Home Kitaifa Ngumu Kumeza iliyogusa Singida United

Ngumu Kumeza iliyogusa Singida United

9782
0
SHARE

Tukiwa njiani tunatokea Mwanza yanatokea mabishano kwenye basi baina ya abiria hiyo ni baada ya mmoja wao kuja matokeo waliyoyapata Yanga dhidi ya Stand United, ni ishara ubingwa unarejea Jangwani bila hofu yoyote.

Mwingine anaibuka anasema Simba wanaache kuchukua kwa ubora walionao? Jamaa mmoja anasema mbio za ubingwa zimebakia kwa timu mbili tu Yanga na Simba, wale Azam wanawasindikiza tu. Konda ambaye alikuwa hataki stori za mpira akauliza hivi wale Sindida United vipi mbona hamuwaulizii au wamepoteana?

Kijana mmoja aliyekuwa amekaa nyuma ya dereva ambaye kwa muda mwingi alikuwa kimya anajinyoosha kisha anasema hiyo Singida United inaniuma sana maana ndio alikuwa mkombozi wetu Singida lakini imeshidwa kufikia malengo na tatizo sio mwalimu tatizo walioaminiwa na Rais wa timu ndio wanaohujumu hiyo timu.

Huenda hata mwenyekiti wa timu hili suala linamuumiza, ngoja niwaambie ukweli, labda hadhi ya Singida inaweza kusalimika na yasije yakatukuta yale ya Mbeya City. Timu kwa inavyoonekana imetekwa na mkurugenzi wake Sanga ambaye anatumika kwenye maeneo mengi ndani ya klabu yeye ndiye mkurugenzi, msemaji bwana fedha, halafu TFF nao wamefumbia macho suala la mtu mmoja kujimilikisha vyeo vingi.

Kwa kifupi anamiliki vyeo vingi kama mchele ambao una matumizi mengi unapika vitumbua, pilau, biriani, mkate wa kumimina na vingine. Anafanya hayo yote huku mwili ukipenda maisha ya Dar roho ipo Singida, huwezi kuongoza timu kwa style hiyo. Mkurugenzi anafanya kila kitu katika timu bila kumshirikisha mwenyekiti likiwemo tukio la kusimamishwa kwa mchezaji Kambale hadi alipoingia kati na kuandikiwa barua ya kuomba msamaha yaishe.

Mmiliki ambaye ni mwenyekiti hana nguvu tena mbele ya Sanga, hali ya kutengwa kwa mwenye timu ilisababisha asusie kuja kwenye mechi ya Simba ambayo walitandikwa 4-0. Mwenyekiti kamkabidhi timu mdogowake Joel Mwandami azunguke nayo lakini mdogo huyo naye kajiweka kando hivi sasa yupo zake Mwanza kajikita kwenye shughuli nyingine.

Tangu mechi ya Yanga sikumbuki ni lini Sanga amerudi Singida, amemwamini meneja kupita kiasi, yeye ndio anafanya karibu kila kitu, meneja ameshindwa na wachezaji wa Singida huenda hata yeye anakereka, haiwezekani kila baada ya mechi ya Singida United wachezaji wanakwenda kupiga ulabu pale Uhasibu na wengine wanaenda klabu kutafuta vya kustarehesha kwa mtindo ule wa usimamizi mbovu wa timu haitakwenda popote.

Wachezaji wa kigeni nao ni chanzo cha mpasuko kwenye timu, wanaleta matabaka kutokana na thamani zao, mfano ma-pro wamepangiwa apartments maeneo ya Mwaja-Veta kule kwa kishua huku wale wazawa wakikaa katikati ya mji maeneo ya Karakakana.

Wachezaji wapo huru kupitiliza wanafanya wanachotaka, kukutana nao bar sio jambo la kushangaza ndoa zisizo rasmi za kufungwa na kuacha ndio usiseme na kama unavyojua dada zetu wa Singida walivyo warembo sijui kama wanawaacha salama. Maana naonaga bodaboda zikipishana zikileta na kuja kubeba warembo yaani zinaleta zinarudisha kwa style ile sidhani kama mazoezi ya yule mholanzi yanaweza kutunzwa kwa maisha ya starehe kiasi kile.

Kuna huyu mtu wa kuitwa Katibu ndiyo nyoka, anajiona kama Rais wa timu, ukimuona sasa hivi hata hata amebadilika mavazi anavaa Kaunda suti na mashati kama Rais wa timu, la kuogopesha zaidi hata yule mtaalam aliyeisaidia timu wakati inapanda Mzenj Abdallah Ally naye kafungiwa vioo kwa madai eti timu ni nzuri na inashinda kwa nguvu zake yenyewe sio ‘holahola’ kuna watu hawaogopi jamani, unamtapeli pesa mtaalam wa tiba asili kweli? Na yeye akakunja roho na kuahidi sare tu kwenye ligi na ikitokea ushindi utakuwa wa mbindeee.

Unaikumbuka ile kamati ya Saidia singida ishinde iliyokuwa na ndugu Omary Kinyeto ilivyojitolea kumaliza ukarabati wa uwanja Namfua pindi wamiliki wa uwanja waliporudi nyuma nayo imejiweka pembeni kutokana na thamani yake kutoonekana tena, ndugu Kinyeto baada ya kutumia fedha zake nyingi kwenye uwanja baada ya kuona timu inajiweza, kwenda kudai haki yake kawekwa ndani wamesahau mema yake yote aliyofanya kwa kujitolea usiku na mchana, hii ni dhambi ambayo inatuumiza kwa sasa na inagharimu mpaka mwenendo wa timu.

Mashabiki wamekata tama kabisa na timu yao ya Singida United na kuna baadhi wamelikumbuka chama lao la wana la wapiga debe la Stand Misuna. Wakati stori zikiwa zimenoga kumbe tayari tulikuwa tumefika Singida mjini na shabiki huyo wa soka akashuka na kutuacha tukiendelea na safari yetu kurudi Dar huku kila mtu akisikitikia maisha ya timu hiyo wengine wakitamani hata wangemlipia nauli  hadi Dodoma aendelee kutpa stori.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here