Home Makala Barua ya Conte kwenye mfuko wa Abramovic

Barua ya Conte kwenye mfuko wa Abramovic

10112
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Hakuna kitu kibaya kama mkeo kugombana na majirani au mawifi. Hiki ndicho kinachomsibu Roman Abramovic. Conte bwana! Dah! Achana na taarabu zake na Jose Mourinho, weka pembeni sakata lake na Diego Costa, Achilia mbali kurupushani lake na Makocha wasaidizi, fukufuku lake na Mashabiki ila hili la vipigo vimenigusa. Kitendo cha yeye kujibizana na mashabiki pale uwanjani mhhhh na bado wametolewa michuano ya UEFA! Hawana uhakika wa kurudi nafasi nne za juu kwa mantiki hii Chelsea UEFA mpaka uchaguzi mkuu 2020.

Antonio Conte ana historia ya kibabe sana. Niwakumbushe kitu, mwaka juzi tu hapo 2010 Conte alikuwa na Klabu ya Atlanta. Timu ilipata Matokeo mabovu. Akaanza ugomvi na bodi. Akawatolea povu mashabiki. Waitaliano si unajua vurugu lao lakini? Basi, kwenye mchezo dhidi ya Napoli, watu wakajaa uwanjani kushangilia Chama lao. He! Hali sio Hali Atlanta wakapigwa nyumbani. Unataka kujua kilichotokea? Twende taratibu.

*Conte mwaka huu hali yake pale Chelsea ni tia maji tia maji. Anadai wachezaji wanaosajiliwa hakuwataka yeye. Yale yale yaliyomkuta akiwa Juventus*

Basi baada ya mechi kuisha Mashabiki kumbe walikuwa na kinyongo chao. Kilichomuokoa Conte kutoka uwanjani salama ni FFU ya Italia. Unaambiwa aliwekewa Ulinzi mkali sana maana watu roho zilichafukwa. Jamaa ana shombo samaki akasome. Kesho yake Conte aliandika barua ya kujiuzulu Atlanta.

Akaenda Juventus. Alipata mafanikio makubwa mno. Lakini mambo yalipoenda mrama hakukiogopa hata kile kibibi kizee cha Turin. Aliwaeleza wazi kuwa wasitegemee chochote. Timu ilimgomea kuwasajili Alexis Sanchez na Juan Cuadrado. waliwasajili Patrice Evra na Coman kwa Jumla ya Euro miliom 28. Walipovurunda kwenye UEFA Conte alisema Juventus walitaka kunywa Chai ya E 100 kwenye mgahawa ikiwa wao mfukoni walikuwa na E10. Pirlo alipoulizwa kuhusu Conte alisema ni Chizi. Unajua kwanini? Twende taratibu.

Wachezaji muhimu wameomdoka Chelsea, Diego Costa na Nemanja Matic pamoja na John Terry yaani ameondoa wachezaji wenye uzoefu wa michezo 667 na imeleta wachezaji wachanga walioshindwa kufanya vyema. Imenunua Drinkwater, Barkley, Morata, Rudiger, Zapacosta na Bakayoko na Giroud.

Conte anasema chaguo lake ilikuwa Romelu Lukaku. Anasema wachezaji wanauzwa na kununuliwa bila idhini yake. Ameanza kugombana na mashabiki na makocha wenzake. Kilichobaki ni nini? Kimebaki kile alichosema Pavel Nedved alipokuwa mkurugenzi wa Juventus. Alijaribu kufunika kauli ya Rais wa Juventus Andrea Agnelli. Agnelli alisema Conte hashauriki. Nedved alidai Kuwa uvumilivu ndio uliomshinda Conte.

Sasa narudi kwenye kauli ya Pirlo. Kama Conte alishindwana na waitaliano wenzake pale Juventus hadi akaandika barua ya Kujiuzulu, Je ataivumilia Bodi ya Chelsea kweli? Je waingereza wakianza porojo zao? Pirlo alisema Conte ni mtu mzuri, ana akili sana lakini ana uchizi wake. Waitaliano ndivyo walivyo. Kwani ina maana humkubuki Genaro Gattuso? Sasa kama waitaliano wenzao wanamuona Chizi na hashauriki tutegemee nini kutoka kwenye mdomo wa Abramovic?
Katika kipini cha miaka 15 abramovic amefukuza makocha 10, na ni kocha mmoja tu aliyeweza kuitumikia Chelsea kwa muda wa zaid ya miaka mwili. . Romani ana hela sana na Conte ana uzoefu wa kuandika barua za kujiuzulu. Nani mshindi hapo? Ukimfukuza unamlipa chake, akiandika barua hapo itabidi mgawane hasara. Ila kwakuwa Conte ni Chizi hashindwi kuandika barua. Nasubiri kuona Je Roman atamfukuza amlipe au Conte atajitoa akili kama kawaida yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here