Home Kitaifa Wambura ana haki ya kukata rufaa?

Wambura ana haki ya kukata rufaa?

4993
0
SHARE
Hamidu Mbwezeleni Mwenyekiti kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF

Mwenyekiti wa kamati ya maadili hamidu amesema baada ya hukumu ya kumfungia maisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura kutojihusisha na  shughuli za soka, Wambura ana nafasi ya kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa na kusikilizwa.

“Nafasi ya kukata rufaa anayo na kamati ya rufaa ipo, kama atakwenda pale anakaribishwa”-Hamidu Mbwezeleni, mwenyekiti kamati ya maadili.

Kwa mujibu wa wakili wa Wambura Bw. Emanuel Muga amesema, mchakato wa shauri la mteja wake haukufuata kanuni wala sheria kufikia hukumu iliyotolewa na kamati ya maadili.

Tuhuma tatu ambazo zilikuwa zinamkabili Wambura ni kupokea ama kuchukua fedha za shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kanuni za maadili ya TFF, kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya Jet System Limited huku akijua malipo hayo siyo halali, shitaka la tatu ilkuwa ni kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya shirikisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here