Home Kitaifa Kijiko cha Wambura kwenye sahani ya TFF

Kijiko cha Wambura kwenye sahani ya TFF

6173
0
SHARE

Na Priva ABIUD
Watanzania ni watu poa sana. Hata mkiwa mnaiba kila mtu akichukua chake bila kumsumbua mwenzke hamna tatizo. ndivyo tulivyo. tumeumbwa hivyo. kigezo ni kwamba watanzania ni wazalendo sana. tunalindana kifupi yani. Ila unapoweka pua kwenye sahamu ya mwenzako hawakuachi salama. Nimejaribu kuangalia hili suala la Michael Richard Wambura Makamu Raisi wa TFF nimebaki njia panda. Watanzania wako hivi: akiwa anakula usishike kijiko chake. Ukimtibua mwenzako atafufua makaburi yako ya zamani. Tumesikia suala la Wambura lina miaka zaidi ya 5. Unaweza kushangaa. Mtanzania ukishika kijiko chake wakati anakula atamwaga chakula chako. Ila swali ni je kwanini ushike kijiko cha mwenzio wakat unajua kabisa una chakula ulificha kwenye kabati? Wambura kwani umewafanyaje wenzio? Watanzania hatuna roho mbaya kiasi hicho kuna mahali umekosea.

Wakati Wambura anapigwa ile marufuku kila mtu alisifia maamuzi ya TFF. Lakini baada ya Wambura kuongea naona sauti zile zimebadilika na kuwa Minong’ono. Dizaini kama kuna ukungu sasa.

Rafiki yangu (jina kapuni) tumesoma wote sheria na kwa bahati nzuri wewe upo hapo TFF kwenye idara ya Sheria na Wanachama. Naomba unisaidie ile kanuni ya Natural Justice (haki ya kusikilizwa) uliyosoma chuo. Ni uatatibu wa gani huu mtuhumiwa anahukumiwa bila kusikilizwa? Au utaratibu wa kutimua watumishi hewa nao imetumika huko? Mnataka kuniambia TFF mnatumia (Summary Dismissal) siku hizi au naota? au Wambura anacheza na akili zetu?

Kwani hili suala la Wambura ni la kisiasa nalo? Hata ingekuwa ni la kisiasa je kwenye siasa nako utaratibu hakuna? Kwani kwenye idara za Siasa mtu hasikilizwi? Rafiki yangu naomba unisaidie kumuuliza Allan Kilivia je hawa waliomhukumu Wambura walikuja ofisini kweli? Kama walikuja basi wameaibisha taaluma ya ofisi yenu.

Samahani lakini, kwani hao hapo ofisini wote si mmepata digrii ya Sheria?

Poleni sana idara ya sheria na wanachama TFF. Labda niseme hili suala limekaa kisiasa (siasa namaanisha vululuvululu) kama Wambura anavyoituhumu kamati husika.

Mwanasheria mwenzangu kwenye sheria sikuwahi kusoma kitu kinaitwa “MKAKATI” nimemsikia Wambura akisema hili suala ni la kimkakati.

nanukuu “suala la kughushi nyaraka linapaswa kuchunguzwa na jeshi la Polisi na hiyo Kampuni inayosemekana nimechukua hizo pesa si ina Wakurugenzi kwanini wasiitwe waulizwe kama ni kweli au”.

“Ndio maana nasema hili ni suala la kimkakati dhamira yao ni kunitoa kwenye nafasi lakini bado halikwisha nasubiri waniandikie barua rasmi’ haya ni maneno ya Wambura

nimewaza sana kuhusu hili neno mkamkati. Hata mimi ningekuwa hapo ofisini ningeshindwa kuwashuri kuhusu mkakati maana sisi  hatujawahi kufundishwa hicho kitu. Sijajua kama mmefundishwa hizo kanuni za kuendesha vikao vya mkakati. Labda sisi wa chuo cha kata huo mtaala haujafika. lakini sheria za TFF zinasema mtuhumiwa anafikishsiwa barua ya wito ofisini na sio nyumbani. tena anapswa apewe siku tatu za kujiandaa vipi kaka hili nalo liemkaaje?

Inawezekana hata wewe ulishindwa kuwashauri namna ya kuendesha mkakati. Nina amini hivyo. au Wambura ameshika kijiko cha Mwenzake?

Pia naomba nikung’ate sikio rafiki yangu “Waambie watu wa idara yako kwamba, mtaani kuna fununu (hearsay), wanasema kuna nongwa huko.kuna mtu anaitwa Cliford Ndimbo hebu ongea nae vizuri. mchunguze sana huenda anajua mengi. pia kuna tetesi kwamba nasikia ni kaimu katibu mkuu ana habari nyingi zaidi kuhusu hili… au tuachane nao nikuulize kitu, kuna vyeo Fulani Fulani viko hapo ila inasemekana vimetolewa kwa wahusika kupitia kwa mlango wa uwani. Wadau wanasema hazikutangazwa watu walipelekewa fomu nyumbani kwao kama kadi za mwaliko wa Harusi. Na mdukuzi wangu pia anasema kuwa kuna watu walitaka nafasi ya Wambura.

Pia yawezekana huyu mwanasheria wa Wambura katudanganya watanzania. Kuna uwezekano Wambura amesikilizwa. Huenda tuhuma zake ni siasa za maji taka. Ila kama huyu wakili wake ametudanganya basi hafai na ni kupuuzwa. Anarudisha nyuma maendeleo ya soka.

nanukuu Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona”-Emanuel Muga, Wakili wa Wambura. au huyu nae tumpuuze?

Pia ningependa kufafanuliwa hili kosa la tatu.

Makosa anayoshtakiwa Wambura ni

1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013

2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013

3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

hilo kosa la kushusha hadhi ya TFF ni lipi? kama ni hayo ya juu basi basi kuna kosa kubwa hapo kwenye tafsiri. kwanza kama umemhukumu mwizi kwa wizi huwezi tena kumhukumu eti kwa kosa la kuhamisha mali ya mtu bila ridhaa yake. kimsingi hapo naona kushusha heshima ya TFF ina tafsiri tofauti kabisa na makosa ya hapo awali na ni vyema mngeyaainisha ni yapi. mtu atahukumiwa kwenye kosa moja mara mbili au zaidi endapo tu hilo kosa linatambulika kwa sheria mbili tofauti na sivyo mlivyoelezea hapo juu.

pili je vipi kuhusu uwezo wa ile kamati kumjadili? anasema yeye ni kiongozi mkubwa. “”Mimi ni Makamu wa Rais siwezi kupelekwa kwenye kamati ndogo kama ile kwa mujibu wa katiba ya TFF ilipaswa nipelekwe kamati ya utendaji au mkutano mkuu:”.

tatu nauliza

TFF ina mamlaka ya kujadilia masuala ya Rushwa kweli? kaka ile kanuni ya Public Interest hapa haihusiki kweli? tokea lini TFF ikajadili suala kubwa namna hii? yaani bodi za kiutawala leo zinajadili uhalifu mkubwa namna hii?

kumbuka hizo ni tuhuma za awali hearsay kaka ( maneno ya kusadikika lakini) Mwisho kaka nikudodose tu idara yenu imedharaulika sana. Na kibaya zaidi inadharaulika mara mbili. Inadharaulika mtaani na wahusika waliotoa Maamuzi wameidharau nafasi yenu. Nyie ni wajuvi wa sharia, je haya maamuzi yanayokingiwa kifua na Wamburi yapo kisheria? Je nyie ndo mmeshauri hivyo? Nina uhakika wewe na kaimu mkurugenzi hamjashauri haya. Sasa shida inakuja kuwa mtaani watu watasema wanasheria wa TFF ovyo kabisa. Kumbe huenda mliwashauri vyema.

Na kama hawakuomba ushauri wa kisheria kwenu basi hiyo idara yenu haina maana yoyote hapo TFF na kama mliwashauri vyema na wakakengeuka pia bado wamewadharau. Ina maana gani sasa kama mambo ya kisheria mnayaongoza kimkakati? Sina uhakika kaka ni fununu za Mdukuzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here