Home Kitaifa Kocha Mbao afunguka kuhusishwa kujiunga Yanga

Kocha Mbao afunguka kuhusishwa kujiunga Yanga

10451
0
SHARE

Kama ni mfuatiliaji wa mambo, utakuwa unakumbuka kuhusu kocha mkuu wa Mbao Etiene Ndayiragije kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Yanga baada ya aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi kuamua kukaa pembeni.

Ilielezwa kuwa, Yanga ilikuwa ikihitaji huduma ya Etiene ili achukue nafasi ya Mwambusi lakini kocha huyo raia wa Burundi alikataa kwenda Yanga kuwa msaidizi wa Lwandamina badala yake akasema kama mabingwa watete wa VPL wanamhitaji, atakuwa tayari endapo watampa nafasi ya kuwa kocha mkuu.

Sasa kocha huyo amevunja ukimya na kuamua kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo kama linaukweli wowote au zilikuwa ni tetesi.

“Siwezi kusema chochote kwa sababu mimi nina   ‘management’ yangu, sijui kama wamewahi kukutana na watu wa Yanga kwa ajili ya jambo hilo”-Etiene Ndayiragije.

“Mimi huwa napewa taarifa jambo likisha kamilika sio tetesi, nadhani jambo hilo halikukamilika ndio maana hata sikupewa taarifa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here