Home UEFA Champions League Hali ni tete Robo fainali UEFA

Hali ni tete Robo fainali UEFA

14249
2
SHARE

Tuachane na hayo yaliyotokea. Haya nayo yanapita. Robo fainali hii hapa. Uingereza ina timu mbili tu kati ya tano. Kila mmoja anatamani apangiwe na Sevilla au Roma au hata Liverpool. Hizi ndio timu ambazo angalau hazina presha kubwa. Kuna baadhi ya watu wanaombea mchezo wa Man City na Barcelona utokee. Binafsi yangu nina amini huo ndio mchezo mgumu kuwahi kutokea katika kipindi cha hivi karibuni.

Kuna baadhi ya timu ngumu ambazo hazipaswi kukutana mapema. Barcelona dhidi ya Buyern, Barcelona Dhidi ya Man City na Barcelona dhidi ya Real Madrid au Real Madrid dhidi ya Man City au Real Madrid dhidi ya Buyern. Robo fainali za mwaka huu ni ngumu sana. Baadhi ya vilabu havijakutana na timu ngumu sana.

Tumeshuhudia baadhi ya matokeo ya kushangaza mengi yametokea, kama Real Madrid kufungwa na Tottenham kisha Tottenham kupoteza nyumbani na Juventus, PSG kumfunga Buyern kisha PSG kufungwa na Real Madrid aliyepigwa na Tottenham, Chelsea kutandikwa na Roma kisha Roma akapigwa ugenini na Shaktar Donestik. Kimsingi kumekuwa na sintofaham sana.

Timu nyepesi zipo mbili mpaka tatu (Sevilla, As Roma na Liverpool) hizi timu kama hazitokutana wenyewe kwa wenyewe hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kufuzu ispokuwa Liverpool itategemea watakutana na nani. Nina imani kati ya mambo yafuatayo.

Liverpool anaweza kufika fainal na anaweza kutwaa ubingwa huo endapo bahati itangukia kwao. Barcelona haitishi kama hapo awali na ikikutana na wafuatayo itatoka (Man City na Buyern).

Changamoto kwa Guardiola
Man City haijakutana na changamoto yoyote uefa na kama watakutana na Buyern au Madrid siwapi nafasi ya kupita.

Mtazamo wangu juu ya Liverpool
Narudi kwenye mantiki yangu dhidi ya Liverpool. Kama Liverpool itakutana na Sevilla au Roma au hata Buyern watasonga mbele. Safu ya ushambuliaji ya Liverpool ni hatari sana kuliko safu yoyote msimu huu. Walio wengi wanaamini uefa ni uwezo. Sawa ni kweli ila kuna wakati nafasi unayopata inakuja kama bahati. Kwa mfano inategemea unakutana na nani? Hali ya hiyo timu kwa wakati huo (majeruhi/ufanisi wa timu)

Historia je?
Liverpool mwaka 2004 ilifanya maajabu makubwa mno licha ya kufungwa mechi 14 kwenye ligi. Mfungaji wao bora alikuwa Milan Baros magoli 13 michuano yote. Walipigwa nje ndani ya Chelsea lakini kwenye hatua ya mtoano Uefa waliwatoa Chelsea na Juventus. Nina imani kuwa kama watapata nafasi basi watafika mbali.

Itategemea sana watakutana na nani. Wakikutana na timu dhaifu kwenye kuzuia watafanya makubwa. Jurgen Klopp aliwahi kufanya makubwa akiwa na Borussia Dotmund ambayo haikuwa na jina kubwa sana UEFA. Mpira ndivyo ulivyo isishangae Liverpool kutwaa Ubingwa au kufika mbali. Baadhi ya timu zinajikongoja sana. Waangalie Juventus walivyotolewa Jasho na Tottenham. Kwenye ligi wananyang’anyana mfupa na Napoli. Waangalie Vizuri Madrid hawapo sawa sana. Tishio kubwa kwa Liverpool ni Buyern na Barcelona ambao hawajakutana siku za hivi karibu na zipo kwenye kziuri.

Barcelona inapata matokeo lakini inaonekana ni mgongo wa Messi zaidi. Kwa uchezaji wao ukimtoa Messi basi hakuna Barcelona. Madrid wanajua fika hawana kombe lingine wagapigana kufa na kupona.

Toa utabiri wako wa hatua hii ya robo fainali

Comments

comments

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here