Home Kitaifa Tshishimbi alivyomtupa Okwi tuzo ya mchezaji bora

Tshishimbi alivyomtupa Okwi tuzo ya mchezaji bora

8987
0
SHARE

Kiungo wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi ametangazwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa ligi kuu Tanzania bara.

Tshishimbi amewabwaga Pius Buswita (Yanga) na Emanuel Okwi (Simba), lakini mchuano mkali ulikuwa ni kati ya Tshishimbi na Okwi.

“Katika mwezi huo ambapo mechi nne zimechezwa Pius Buswita alifunga magoli mawili na kuisaidia timu yake kupata pointi 12 kwa upande wa Tshishimbi katika mechi nne aliisaidia timu yake kupata pointi 12 na kufunga magoli matatu na assist moja.”

Emanuel Okwi alifunga magoli manne katika mwezi huo na kuisaidia timu yake kupata pointi 10.

“Kwa hiyo kamati ya tuzo baada ya kupitia vigezo mbalimbali kwa wachezaji hao watatu mwisho ikamtangaza rasmi mchezaji bora wa mwezi Februari wa ligi kuu Tanzania bara ni Papy Kabamba Tshishimbi.”

Atapata shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi kampuni ya Vodacom, atapata pia king’amuzi cha Azam TV ambao ndio warushaji wa michezo ya ligi lakini atapewa tuzo maalum kutoka TFF.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here