Home Makala Mastaa Hawa wamefulia, wanatangatanga

Mastaa Hawa wamefulia, wanatangatanga

11615
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Ngoma ikipigwa sana mwishowe inapasuka au inakosa ladha yake ya hapo awali. Kuna baadhi ya mastaa kipindi cha nyuma walitesa sana na vilabu vikubwa barani ulaya lakin kwa bahati mbaya kwa sasa hawana vilabu maalumu na hawana mikataba kabisa. Katika orodha hii wapo mastaa wakubwa waliowahi kutamba ligi kuu England, Hispania, Ufaransa na Ujeruman. Takwimu pia zinaonesha mastaa wengi wanaondoka kwenye kikosi cha Arsene Wenger wengi wao wanaonekana kupata mafanikio ambayo aidha yanakuwa ya muda mfupi au ambayo hawajawatumikia sana.

Marouane Chamakh

Samir Nasri
Baada ya mizunguko mingi katika nchi za Hispania na England kwa sasa Nasri hana timu ya kucheza. Kwa bahati mbaya zaidi amepigwa marufuku ya kutojihusisha na soka kwa muda wa miezi 6. Nasri alifanya vyema sana katika kikosi Cha Arsenal kitendo kilichomfanya apachikwe jina la Zidane Mpya. Nasri kabla ya kupigwa marufuku alijiunga na klabu ya Antalyspor ya uturuki lakini baada ya kuichezea michezo nane pekee aliamua kuachana na klabu hiyo na kuwa mchezaji huru. Kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote.

Anderson
Mashabiki wa Man United watamkumbuka vyema kiungo huyu machachari kabisa aliyetamba kwenye kikosi cha Sir Alex Ferguson. Baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza, alivunja mkataba wake na Man United na kwenda nchini Brazil kwenye klabu ya Internacionale. Baadae alitupwa Coritiba kwa mkopo. mkopo ulipoisha alirudi klabuni hapo kisha kuvunja mkataba wake na Internacional. Mpaka sasa hajaongeza mkataba na hajataja ni klabu ipi atakwenda Anderson bado umri wake unamruhusu kufanya makubwa kwani ana umri wa miaka 29 tu.

Marouane Chamakh
Mwezi wa tano mwaka 2010 Chamakh alijiunga na Arsenal akitokea ufaransa kwenye klabu Bordeaux. Aliisaidia Arsenal kutwaa ubingwa wa Carling. Pia aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kwenye michuano ya UEFA kufunga magoli 6 kwenye mechi 6 mfululizo. Baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye misimu iliyofuata alipelekwa West Ham kwa Mkopo, kisha alitimkia Crystals Palace, na hatimaye Cardiff. Alifanikiwa kuichezea Cardiff michezo miwili pekee yote akitokea benchi. Desemba 2016 Cardiff ilivunja nae mkataba na kufikia sasa hana mkataba na klabu yoyote. Chamakh Raia wa Morocco atakumbukwa vyema kwa muonekano wake ambao wengi walimfananisha na Cristiano Ronaldo. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufunga magoli ya kichwa.

Alex Song.
Moja ya viungo bora kabisa katika dimba la katikati ambaye kwa miaka 10 iliyopita mashabiki wa Arsenal hawawezi kumsahau. Baada ya kashkashi na kocha wake Arsene Wenger, Song alitimkia Barcelona kwa malengo ya kutwaa Mataji. kutokana na kukosa nafasi ya kudumu kule katalunya maisha ya benchi yalimzonga sana Song. Hali yake Barcelona haikuwa njema kutokana na ushindani mkubwa kwenye kikosi cha Barcelona. hali hii ilimfanya kutolewa West Ham kwa mkopo lakini bado hakuweza kuonesha makali yake ya hapo awali. Raia huyu wa Cameroon tokea aliposafiri kutoka kwenye mikono ya Wenger ameishia kuonekana mzururaji tu. licha ya kwamba alikuwa na kiwango bora kabisa lakini kiufupi amefulia.

Luis Fabiano.
Ukizunguka Miji ya Ivory Coast ukatamka jina la huyu jamaa unaweza ukapigwa mawe. Mwaka 2010 aliwafunga goli la dhuluma kwa kushika mpira mara mbili lakini mwamuzi hakuona na kuweka mpira kimyani. Ni moja kati ya wachezaji wakukumbukwa na mashabiki wa Seville. kati ya washambuliaji waliokosa bahati kwenye kikosi cha timu ya taifa basi ni huyu. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 lakini bado anadai kuwa ana uwezo wa kupambana uwanjani. Amewahi kucheza pia china katika klabu ya Tijan kabla ya kurudi Vasco Da Gama ambapo amemaliza nao mkataba. Kwa sasa hana mkataba wowote huenda tutegemee lolote kutoka kwake.

  • Jackson Martinez
    Alitajwa kuwa moja ya lulu murua kwa wakolombia. Alipokuwa Porto alifanya mambo makubwa sana. Kiwango Chake kilikuwa cha kuvutia kiasi cha kuwatamanish”a Mabosi wa Atletico. aliifungia Porto Magoli 94 kwenye michezo 142. Alipokiunga na Atletico aliifungia magoli 3 kwenye michezo 22. klabu ya Guanzhou Everngrade ya China ilimnunua kwa kititia cha Euro Milioni 42. hivi majuzi taarifa zinadai klabu hiyo imeamua kumtimua. Alijulikana kwa jina la utani “Cha Cha Cha” kutoka na uwezo wake mkubwa wa kufunga. Kwa sasa amefulia hana jipya tokea akimbilie huko kwa wachina. Ana umri wa miaka 31 lakini tayari ameshapoteza ladha yake. Alikuwa na ujuzi na ufundi wa kuchezea mpira utadhani anacheza muziki

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here