Home Kitaifa Makamu wa Rais TFF kujadiliwa kamati ya maadili kwa tuhuma tatu

Makamu wa Rais TFF kujadiliwa kamati ya maadili kwa tuhuma tatu

7789
0
SHARE

Shirikisho la soka nchini TFF limesema Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura amefikishwa kwenye kamati ya maadili kwa ajili ya kujadiliwa kutokana na tuhuma tatu tofauti anazokabiliwa nazo.

Tuhuma zinazomkabili Wambura ni kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali, kughushi barua pamoja na kushusha hadhi ya shirikisho hilo linalosimimia soka nchini.

“Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana leo Jumatano Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili, akikabiliwa na makosa matatu.

  1. Kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali
  2. Kughushi barua ya kuelekeza malipo ya kampuni ya Jeck System Limited
  3. Kushusha hadhi ya shirikisho (TFF)

Makosa hayo yote ni kinyume na kifungu cha 73(1), 73(7) ya kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013 na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF 2015.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here