Home Kimataifa Lionel Messi “La Pulga” awafungashia virago Chelsea

Lionel Messi “La Pulga” awafungashia virago Chelsea

7543
1
SHARE

“Yule hamna kitu.. ajee England tumuone. La liga mbovu tu. Ligi ya watu wawili. Barca akija England hata kwa Stock City anakaa”

Hizi ni mojawapo ya kauli nyingi za kishujaa ambazo zimezoeleka na mashabiki wengi wa soka duniani. Tuachane na Hayo. Messi ametimiza magoli 18 kwenye michezo 20 dhidi ya timu za Uingereza. Timu za Uingereza zilizoshiriki uefa mwaka huu zilikuwa 5 na zilizofanikiwa kusonga mbele ni mbili pekee yake.

Yule Messi ambaye ilisemekana hawezi kuifunga Chelsea leo ameweka rekodi yake murua kabisa ya kufunga goli la mapema kabisa katika historia ya Maisha yake. Goli la dakika ya pili limefanya Messi aweke rekodi hiyo. Messi ametimiza idadi ya magoli 100 huku akifanikiwa kuitoa Chelsea katika Michuano ya UEFA. Chelsea walifanikiwa kupata sare ya bao 1-1 katika jiji la London lakini walipokwenda Mjini Barcelona kibao kimegeuka. Magoli mawili kutoka kwa Lionel Messi na moja la Ousmane Dembele limetosha kuwarudisha vijana wa Antonio Conte mikono mitupu.

Messi waliwatanguliza Chelsea London kwa goli zuri la tobo kunako dakika ya pili na kuvunja rekodi yake ya hapo awali ya kufunga goli dakika ya pili na sekunde ya 28. Chelsea walipiga mashuti 7 matatu walilenga golini, Barcelona walilenga shuti moja nje na mashuti 7 walilenga goli. Makosa madogo madogo ndiyo yaliyowagharimu chelsea. Inaonekana kitendo cha Chelsea kuamua kucheza mpira dhidi ya Barcelona kwa kufungua nafasi kuliwaponza sana.

Messi amefikisha magoli 100 ya uefa katika michezo 123 akimfukuzia Cristiano Ronaldo mwenye magoli 117 katika michezo 143. Messi alishindwa kufunga katika michezo 8 ya hapo awali dhidi ya Chelsea. Barcelona sasa wataungana na Buyern Munichen, As Roma, Seville, Manchester City, Liverpool na Juventus katika hatua ya Robo fainali.

Conte ameamua kumwanzisha Oliver Giroud akiamini atafanya kitu. Willian na Hazard walitumika kutengeneza nafasi lakini safu ya ulinzi wa Barcelona ilisimama imara. Cesc Fabregasi ametoa zawadi ya goli kwa Dembele kwa kupoteza mpira ambao messi alikimbia nao na kumtengenezea Dembele goli.

Kwa kiasi fulani Chelsea walichezea mpira na kuonesha uthubutu kujaribu kupambana na Barcelona lakin bahati haikuwa kwao. Huenda Chelsea akashiriki michuano hii mwaka 2019/2020 kwani hali yao bado ni tete. Nafasi ya 4 imekuwa mtihan kwa Antonio Conte.

Droo ya michuano hii itafanyika mapema ijumaa keshokutwa kule jiji Nyon Uswis. Kwa utabiri wako weka koment yako.

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here