Home UEFA Champions League Je Chelsea watatumia leseni ya babu kupaki basi Camp Nou

Je Chelsea watatumia leseni ya babu kupaki basi Camp Nou

6594
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Mtu anapokwambia Chelsea ni Mbabe wa Barca unapaswa umuulize uliwahi kushinda Camp Nou? Kisha muulize, Kutoa sare Barca darajani ndo umeshakuwa vibonde? Enewei Wako sahihi kwa sababu watajitetea walipata suluhu Camp Nou na walishinda mchezo wa kwanza pale Stamford bridge mwaka 2012, kwa hiyo na mwaka huu historia kwao itajirudia, madai yao. Ila tuangalie 2012 barca walikuwaje. Kwanza hawakutwaa laliga. Walifungwa na Getafe, Ossasuna, Na Real Madrid alipata matokeo Camp Nou. Walidroo na villareal, Espanol, Real Sociedad, Real Madrid. Haikuwa kwenye wakati mzuri sana. Chelsea nayo haikuwa na msimu mzuri walifungwa mechi 10 ligi kuu.

Ni kipindi ambacho Guardiola alisumbuana na Bodi kuhusu usajili. Msimu ule Barcelona na Chelsea Ni walevi walikuwa wakisindikizana nyumbani. Baadhi ya mashabiki wa chelsea wanaamini wataifunga Barca au kupata suluhu ya magoli zaidi ya mawili. Sawa wapo sahihi, mpira ni mchezo wa makosa lolote laweza tokea. Tunasemaga mpira una dunda. Wanasema Barca ni mbovu msimu huu haina makali sana. Swali ni je wao chelsea wapoje? Wamefungwa na Burnley, Palace, Man City, West ham na Man United, usisahau na Fc Bournemouth na kaka zetu Watford. Mbaya zaidi wamepigwa na Roma huko Uefa kipigo cha nguruwe kunusa Baibui la mke wa shekh. Istoshe hawana uhakika wa ubingwa msimu huu. Kapitwa zaidi ya alama 26 na kinara wa ligi. Tena kwa aibu akiwa bingwa mtetezi. Chelsea imefunga magoli 52 na kufungwa 27.

Wanasema wanahistoria. Nimejaribu kuangalia timu yao. Wachezaji walioitoa Barca 2011 na hiki kikosi chao cha sasa. Ukiniambia una historia ya kumfunga Barca na unataka kutumia kigezo hicho hicho kwenda kupata ushindi Camp Nou mhh siwezi kukuelewa. Lazima tuangalie uwezo wa timu zote kwa wakati huu na sio Historia, kama ni Historia hayo masuala mtafute Nyambari Nyangwine mtaelewana.

Ni kweli Barca ilipata wakati mgumu sana kwa Chelsea kwenye mchezo wa mwisho, lakini je watacheza hivi hivi Camp Nou? Kama watajizuia basi Barcelona nao watatafuta suluhu ya bila kufungana. Nilichokiona kwa Chelsea ni ugeni wa wa wachezaji wake. Wachezaji wengi ni wapya wachache sana wa uzoefu na uefa. Mwezini sio duniani. Stamford sio Camp Nou. Hupaswi kuishi kwa mazoea. Mkitumia hizi falsafa ni sawa na kuendesha gari na leseni ya babu yako.

Barcelona ni kweli imepungua kasi yao sio ile ya Guardiola lakini mpaka sasa hawajafungwa mchezo hata mmoja. ni kweli barca haitishi sana Hata kwenye mchezo wa mwisho ilionekana wazi Barcelona walikosa mbinu mbadala ya kupenya lango la Chelsea. Lakini swali ni je Chelsea wao watatumia mbinu gani kupata goli Camp Nou? Kama ni kuvizia ni ngumu sana maana Barcelona wao hawana haja sana kupata goli maana tayari wapo mguu mmoja mbele kwa goli la ugenini. Chelsea wao itawabidi watoke nyuma kutafuta goli. Ukitoka nyuma ukiwa unacheza na Barcelona ni sawa na kuotesha miwa karibu na shule ya msingi.

Lakini bado ukiangalia uwezo wa Barca na chelsea ni sawa na mtu mweusi kujifananisha rangi na mzungu muuza mkaa. Mfumo wa Chelsea wa kupaki mabasi uliwasaidia sana. Conte anapaswa atafute njia mbadala kuhakikisha ngome yao haipenyeki tena Camp Nou na kwa namna gani apate goli. Barca ni mbovu lakini sio mbele ya chelsea. Labda turudi kule kule mpira una dunda.

Naona mnajificha kwenye mwamvuli wa historia kuliko uwezo. Sawa jaribu kupaki basi na leseni ya babu. Mnaweza kufanikiwa maana kuna wakati konda anapewa gari na anafikisha abiria salama. Chelsea wana faida ya mambo yafuatayo, Morata tayari amekwisha fika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani ulaya akiwa na klabu ya Juventus, wana Cesc Fabregas tayari amekwisha cheza vilabu vikubwa barani ulaya kama Barcelona na Arsenal. Wengine ni ubora wa kipa wao, umahiri wa mabeki wao wa pembeni.

Matarajio yangu ni Barcelona kutafuta funguo za geti katika mchezo huu. Funguo hizo wanazo Kante, na Drinkwater na hawa hawa ndio watakaotueleza kwanini Messi asipate goli tena. Mara nyingi safari ya Barcelona inaanzia katikati ya uwanja.

Ukitaka kutawanya kiungo cha brceloina Adrien Rabiot, Blaise Matuidi, and Marco Verratti, hawa ndo waliweza kutawala ufalme wa Iniesta wakala 4 kwa mtungi. Paulinho amekuja kuongezeka kwenye utafutaji wa ufunguo. Akiweka rekodi yake katika maisha yake ya kucheza michezo 23 bila kuonja kipigo. Usajili wake million 35 akiwa na miaka 29 ulishangaza wengi na kiwango chake pia bado kimendelea kushangaza.

Pambane kwa uwezo wenu msitumie historia. Kila kheri kwenu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here